November 13, 2012

Mkuu wa mkoa: Awaka kuhusu Viongozi wanaofuja miradi ya wananchi-Muleba

Aliyesimama:-Mkuu wa Mkoa wa kagera kanali Mstaafu Fabian Massawe


Na Shaaban Ndyamukama -Muleba
Zaidi ya shilingi milioni 800 zimefujwa na idara mbalimbali za  halmashauri ya wilaya muleba mkoani kagera kwakujenga  na kuidhinisha malipo ya miradi ya maendeleo iliyo  chini ya viwango 

Mkuu wa mkoa wa kagera kanali mstaafu Fabiani Masawe amesema fedha hizo ni za mradi wa maji wa kijiji cha Buyaga kata ya Buhangaza  na fedha za mradi wa  ujenzi wa hospitali ya wilaya ambapo wakandarasi na wahandisi ndio  wanaohusika na upotevu wa  fedha za miradi hiyo

Kanali Masawe  amesema kuwa  wanaotuhumiwa katika kuhujumu miradi ya maendeleo ya wananchi wilayani muleba ni idara ya fedha  TASAF na uhandisi   na ametoa muda wa siku tatu kwa  wakuu wa idara hizo kukamatwa ili kufikishwa kwenye vyombo vya sheria 

Akitoa majumuisho ya ziara yake katika miradi ya maendeleo wilayani Muleba  Kanali masawe amewataka viongozi wa wilaya hiyo wakiwemo madiwani kufanya kazi kwa uadilifu vinginevyo ataacha kwazi kwa kuondoka na watendaji  wanaofuja fedha za serikali na  mali za wananchi   

Alisema miradi mingi imekwama kwa kuwa wanaoisimamia na kuchukua mikataba ya kuijenga nai watumishi wa halmashauri wakiwemo madiwani na walio wengi hawana taaluma katika fani ya ujenzi na wanatumia fedha za wananchi kujinufaisha 

Alisema kuwa katika ubadhilifu huo miradi ya majengo ya serikali hasa nyumba za watumishi  zahanati shule za msingi na sekondari barabara na madaraja yake huku fedha nyingi zaidi ya milioni 240 zimetumika kulipa malipo hewa kwa watumishi waliohusika kuhujumu miradi mbalimbali

“Kinachoshangaza mambo haya yanafanyika na idara ya ukaguzi wa mahesabu ya ndani ikiwemo na kuona madudu hayo huku TAKUKURU mkiwa maeneo haya leo katika kuacha kazi naondoka na mtu”.Alisema kanali Masawe

Alisema   kufuatia hali hiyo ameunda kamati  ya kuchunguza walioidhinisha fedha  hewa za miradi mbalimbali  ili watakaobainika kufanya kazi bila uadilifu katika kazi zao wakamatwe na vyombo vya dola na wafikishwe  mahakamani na waliokimbia au kuhamishwa wafuatwe walipo kutoa maelezo ya fedha hizo

Alisikitishwa na baadhi ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa hivi karibuni wilayani humo kukutwa na vyufa katika kuta na kupasua sakafu zake huku baadhi ya majengo kujengwa chini ya viwango na tayari waliohusika na ujenzi huo walishalipwa fedha na kuondoka bila kazi kukamilika 

 Aidha Diwani wa kata ya Muleba mjini kupitia chama cha wananchi CUF  Hassani Ramadhani Millanga amemuomba mkuu wa mkoa kuunda kamati nyingine ya kuwachunguza watumishi wa idara zote katika halmashauri hiyo ikiwemo idara ya fedha na elimu kwa kulipa mishahara watumishi hewa ambao hawako kazini aidha kwa kustaafu, kufariki na vinginevyo

Diwani huyo alisema katika usimamizi wa mitihani wanatumika watu ambao ni vibarua na  fedha nyingine zaidi ya milioni 40 zimeibiwa na idara hizo kwa kufuja malipo  wanayodai walimu katika halmashauri ya wilaya hiyo

Alisema kuwamba  kufujwa kwa fedha hizo kunawafanya wakazi waishio visiwa vya kelebe Goziba, Ikuza, Bumbile na visiwa vinginevyo katika ziwa Victoria wilayani muleba wanakosa huduma za kijamii kama miundombinu halisi ya elimu afya barabara ulinzi na usalama licha ya visiwa hivyo kutoa mapato mengi kwa halmashauri kutokana na shughuli za uvuvi.
                                     www.ngarakwetublogspot.com

No comments:

Post a Comment