Awilo Longomba |
WASWAHILI WALISEMA, PENYE NIA PANA NJIA.
NI MSEMO WENYE KUTIA MOYO….
Naomba niutolee Mfano mzuri
msemo huo kwa Mwanamuziki kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC zamani
ikijulikana kama ZAIRE ambaye alianza kama Mpiga Ngoma hadi katika Usupa staa…………
Wengi tumemzoea kwa jina la Awilo
Longomba. Huyu ni miongoni mwa wanamuziki wanaotamba
Afrika na hata nje ya bara hili. Ndoto zake katika Muziki zilianzia katika
upigaji wa ngoma katika bendi za Congo kama vile Viva la Musica ya Julius Wemba diuoshungu maarufu kama Papa
wemba, Stukas, Nouvelle Generation na Loketo inayoongozwa na Arlus Mabere.
Mwaka wa 1995, Awilo aliamua kuachana na kazi aliyokuwa
akiifanya ya kupiga Ngoma(Drum Boy) na badala yake akuamua kuimba. Alifanikiwa kutimia
azima yake,kwani mwaka huo huo alitoa albamu yake ya kwanza iliyoitwa Moto
Pamba, akipata kutoka kwa watu kama akina Shimita El Diego, Ballou Canta, Dindo Yogo, Dally Kimoko, Sam Mangwana, Syran Mbenza na Rigo Star.
Album yake ya pili,iliitwa Coupe Bibamba
ambayo aliitoa mwaka 1998. Na hii ndio
iliyomtamburisha katika anga ya Muziki kote barani Afrika, Ulaya na Amerika. Hii
ilifuatiwa na Kafou Kafou mwaka wa 2001 na albamu yake ya hivi karibuni, Mondongo
mwaka wa 2004, ambayo
inawashirikisha Japponais, Dally Kimoko, Caen Madoka, Djudjuchet, Josky
Kiambukta na Simaro Lutumba. Pia alishirikishwa kama atalaku (mtu wa
kutumbuiza) katika baadhi ya rekodi za soukous.
Awilo kwa sasa anaishi nchini Ufaransa na inasemekana ana
uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Barbara Kanam.
Ndugu zake wengine katika sanaa muziki ni
pamoja na baba yake Victor Longomba mwanachamana mwanzilishi wa TP OK Jazz na vilevile Longombas ambalo ni kundi maarufu la
afro-fusion lenye makao nchini Kenya.
Mnamo mwaka wa 2008 Awilo Longomba alitoa albamu nyinginealiyoiita
SUPER-MAN, ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa.
Umaarufu wake sio tu katika Bara la Afrika bali hata Marekani / na kanada
ambako amefanikiwa kufanya matamasha ya kutangaza Album yake hiyo.
Na: Juventus Juvenary. Kwa Msaada wa internet
No comments:
Post a Comment