Na: Shaaban Ndyamukama
WATU saba wanaokadiriwa kuwa na umri
wa miaka kati ya 30 na 40 wamefariki
dunia huku wawili wakinusurika baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama
katika kisiwa cha Hifadhi ya Taifa Rubondo ndani ya ziwa viktoria wilaya
ya Muleba mkoani Kagera
Akiongea kwa njia ya
simu Jumanne wiki hii diwani wa kata ya Ikuza wilayani Muleba Fortunatus
Martha Wazia alisema kuwa watu hao waliondoka katika kisiwa cha ikuza kwenda
kwenye hifadhi ya Rubondo Novemba nane na walipita njia za panya wakiwepa
walinzi wa hifadhi wasije kukamatwa na wamepatikana wakiwa maiti Novemba 10 ya
jumamosi wiki iliyopita
Wazia amewataja
waliofariki dunia kuwa ni Baruya Masala mkazi wa Muganza wilayani Chato
,Alex Mwita mkazi wa Tarime ,Kipara Kasukari
wa kata ya mushabago wilayani Muleba na mwingine amejulikana kwa jina
moja la Niko mkazi wa sengerema
Wengine ni Obedia
Yohana mkazi wa Muganza wilaya ya Chato,Juma Kengere mkazi wa Itale wilayani Chato na wa saba ametambuliwa kwa
jina moja la Robart mwenyeji wa wilayani Biharamulo.Amesema kuwa katika kuopoa
maiti ndani ya maji jumatatu wiki hii waliotambuliwa na jamaa zao
wamesafirishwa kwa kuzikwa walikotokea na maiti tatu ndizo zimezikwa katika
kisiwa cha Ikuza wilayani Muleba
Alisema wavuvi hao
walikwenda kuvua samaki wakiwa ni wavuvi haramu katika hifadhi ya Rubondo na boti yao haikuwa imara ilianza kuvuja
wakati wakirejea kisiwani Ikuza na hatimaye kuzama ndani ya ziwa hilo
nyakati za usiku na wawili kati ya tisa waliokuwa ndani ya boti ndio
walioogelea hadi nchi kavu mwaloni na kutoa taarifa.
"Siku ya tukio kwa maelezo ya
walionusurika ambao hakuwataja majina yao inasemekana hapakuwa na hali mbaya ya
hali ya hewa ispokuwa boti yao haikuwa imara na iliingiwa na maji wakashindwa
kutoa maji hayo na kwa wingi wao na mizigo walianza kuzamana kufariki
dunia."Alisema Wazia
Aidha Diwani huyo
amewashauri wavuvi katika ziwa Victoria kufanya kazi zao kwa kutumia njia
harali na vyombo vyao kukaguliwa na malaka husika ili kuepusha madhara katika vyombo vyao na maisha yao ikiwa
ni pamoja na kuimalika kwa ulinzi katika shughuli zao
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Bw Philipo Karangi amethibitisha kutokea kwa
vifo vya watu hao na kwamba jeshi la polisi linaendelea kufanya upelelezi
kuhusiana na mazingira yaliyopelekea kutokea kwa tukio hilo.
www.ngarakwetublogspot.com
No comments:
Post a Comment