Kainula Aloys |
Na:-Shaaban Nassibu Ndyamukama
Katika kujiinua kimaisha Binadamu
anahitaji kufanya kazi kwa kutumia akili na viungo vyake vya mwili ili
kujikwamua kimaisha katika familia.
Watu walio wengi wamekuwa wakikosa
kufanya kazi kwa kutumia maumbile yao
kwa madai kazi hakuna wakitaka za
ofisini na kulipwa mishahara na serikali au mashirika yakiwemo makampuni.
Pia jamii imekuwa ikiwabeza walio na
hitilafu za maumbile hasa walemavu wa viungo vya mwili kwa kukosa kuwasaidia
katika kujiajiri na kupata riziki aidha mashirika ama taasisi binafsi na
kuwafanya walio na mahitaji maalum kukosa mwelekeo wa maisha
Suala hili limekuwa na mtazamo Tofauti kwa
Baadhi ya walemavu kuwa kuwa nahitilafu za viungo si kuwa omba omba mitaani
waweza kujishughulisha na kazi ndogo na hatimaye kujikwamua kwa kujiajiri na
kupata kipato kinachosaidia kupata fedha nakujijengea makazi bora ukisubiria serikali na taasisi
nyinginezo kuongeza nguvu kwenye juhudi zako.
Hali hiyo nimeikuta kwa mjasiliamali
mlemavu wilayani Muleba anayefanya kazi ya kushona viatu Muleba mjini Bw Aloyse
Kainunula Pichani hapo juu aliyesema kuwa alipata ulemavu wa miguu akiwa mtoto
baada ya kuugua polio na anatembelea kiuno lakini kwa kazi hiyo sasa ana mke na
watoto watatu licha ya kwamba hakujaliwa kwenda shule ya aina yoyote.
Bw Kainunula hapati msaada wowote wa
kijamii anaishi kwa nguvu na maombi ya kutaka walio na viatu viharibike ili
waeze kuletea na kufanya ukarabati kwa kupata malipo ya shilingi 300 hadi 1000
kwa mteja na mtaji wake ni Matairi ya gari yaliyokwisha choka barabarani ili
kuingiza sori na nyuzi za katani anazosokota kushonea viatu hivyo akikosa fedha
za kununulia nyuzi za Nyloni.
Wasamalia wema kama mpo kazi yake
anaifanyia ndani ya bandala magunia machakavu na makasha ya kufungia bidhaa
yaliyochanika lakini akiwezeshwa sehemu nzuri ya kazi anaweza kuhimili mikiki
ya maisha kwani bado ni mdogo ana umri wa miaka 35 tu Mashirika ya kidini yanayotoa
msaada angalieni kiumbe huyo wa Mungu anayeishi Muleba mjini akiwakiwa na jua
la mwaka mzima na kunyeshewa mvua ya mwaka mzima huku tuliojaliwa neema ya
mungu tukipata na kusaza bila kumtole sadaka mungu kupitia kwa malio na
mahitaji.
No comments:
Post a Comment