|
Defender la Polisi likilanda mitaani kuimarisha hali ya usalama na kutuliza fujo |
|
Askari akiendeleza harakati za kuimarisha usalama |
|
Kikosi cha FFU |
|
Hii ndio nyama inayosadikiwa kuwa chanzo cha Vurugu, imechinjwa na wakristu jambo linalipongwa kuwa hawana mamlaka ya kuchinja |
|
Waraka uliohamasisha wakristu kushiriki katika uzinduzi wa siku ya Kuchinja |
|
Majeruhi wa tukio hilo |
|
Kijana aliyejeruhiwa baada ya kupatiwa huduma ya kwanza |
Baadhi ya wakazi wa kata za
Buseresere na Katoro katika wilaya za Chato na Geita wameilalamikia serikali
kushindwa kutoa tamko hali iliyopelkea vurugu na mauaji ya Mchungaji wa kanisa
la P.A.G.T na baadhi ya raia kujeruhiwa vibaya
Wananchi hao wamesema hayo ikiwa ni
siku moja baada ya mapigano ya waislam na wakristo kutokea katika kata ya
buseresere wilayani Chato
Mmoja wa wananchi hao Bw. Paschal
Magoho amesema Serikali ilitakiwa kuchukua jitihada za maksudi mapema ili
kuzuia vurugu hizo
Katika vurugu hizo,Mali za wananchi
zimeharibiwa vibaya huku baadhi ya maduka na bidhaa zikiteketezwa kwa moto
Miongozi
mwa wananchi walioharibiwa mali zao ni Pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la
waislam Tanzania wa wilaya ya Chato na
mwenyekiti wa CCM kata hiyo Bw.Yusuf Idd Banana ambaye ametaja mali
zilizoharibiwa kuwa na thamani ya Shilingi milioni 10.
Ugomvi huo uliosababisha mauaji, majeruhi na uharibifu wa mali umetokana na hoja ya wakristu wakitaka kuwa na mamlaka ya kuchinja mifugo na kupinga dhana kuwa wenye mamlaka ya kuchinja ni waislam pekee, na kwamba waislam wanapochinja wakristu wanakula, jambo ambalo linaelezwa kuwa ni kinyume na wakristu wakichinja waislam hawali!..............................................Eeemungu, tuepushe na dhambi ya UDINI..
Vyombo vingine vya habari vimeandika:-
VURUGU kubwa za kidini kati ya Waislamu na Wakristo, zimezuka katika
kijiji cha Buseresere, wilaya ya Chato, mkoani Geita, na kusababisha
kifo cha Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God, Mathayo
Kachila (45), huku watu wengine 10 wakijeruhiwa vibaya kwa mapanga.
Mchungaji huyo alichinjwa na watu wanaodaiwa ni kuwa waumini wa
Kiislamu kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo
viko jirani na eneo hilo jana.
Taarifa kutoka eneo la tukio hilo zilisema kuwa tukio hilo lilitokea
asubuhi ambapo chanzo chake kinatajwa kuwa ni watu wanaodaiwa kuwa
wafuasi wa Kiislamu kuvamia bucha iliyokuwa ikiwauzia nyama Wakristo wa
kijiji hicho waliokuwa wamepanga foleni kwa wingi kusubiri huduma hiyo.
Wakiristo hao walikuwa wamechinja ng’ombe mmoja na mbuzi wawili eneo
la kanisani kabla ya kuipeleka nyama hiyo katika bucha hiyo iliyoko eneo
la Buseresere Sokoni na ndipo walipokumbana na kadhia.
Mashuhuda walisema kuwa tukio hilo lilianza saa 2:00 asubuhi muda
mfupi baada ya nyama kuwasili katika bucha hiyo ya Wakristo kwa ajili ya
kuuzwa, jambo linalodaiwa kuwakera Waislamu ambao waliivamia bucha hiyo
kwa lengo la kuifunga.
Taarifa ziliongeza kuwa wakati Wakristo wakitafakari uwepo wa Waislamu
kwenye bucha yao, ghafla walishtukia wenzao hao waliokuwa wametapakaa
kwa wingi wakiimwagia nyama hiyo vitu vinavyodaiwa kuwa sumu.
Kutokana na hali hiyo, Wakiristo walioonekana kukerwa na kitendo hicho
na ndipo mapambano yalipoanza kati ya pande hizo mbili huku Wakristo
wakitumia mawe na Waislamu wakitumia mapanga na majambia.
Ilidaiwa kuwa wakati mapambano hayo yakiendelea, mchungaji huyo ambaye
kwa sasa ni marehemu alifika eneo la tukio ili kujua kulikoni na ndipo
alipojikuta akishambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za kichwani na
kupoteza maisha akikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa
matibabu.
“Yaani ilikuwa kama mzaha tu...baada ya Wakristo kuleta ng’ombe mmoja
na mbuzi wawili kwenye bucha yao, tulishangaa kuona Waislamu wamevamia
hiyo bucha wakati tayari nyama ikiwa inauzwa na Wakristo wakiwa
wamepanga foleni wakisubiri kuhudumiwa,” alisema shuhuda mmoja.
Aliongeza kuwa Waislamu walipofika walitaka kuifunga ile bucha lakini
Wakristo waligoma na ndipo wengine walifika na kuimwagia ile nyama vitu
kama sumu na huo ukawa mwanzo wa machafuko.
“Kwa vile wenzetu walifika eneo hilo wakiwa na silaha tayari walianza
kuwakata Wakristo na kuivunjavunja ile bucha huku Wakristo wakijihami
kwa kutumia mawe lakini walizidiwa nguvu,” alisema shuhuda mwingine.
Waliojeruhiwa ni Saidi Ntahompagaze (45), Sadick Yahaya (40),Yasin
Rajab (56),Vicent Damon (22), wote wakazi wa Buseresere na mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina moja la Ramadhan ambaye yuko mahututi katika wodi
namba nane katika hospitali ya wilaya ya Geita.
Hata hivyo watu wengine watano ambao majina yao hayakuweza kupatikana
mara moja walitibiwa na kuruhusiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri.
Polisi kutoka wilaya za Chato na Geita walifika eneo la tukio hilo saa
4:30 na kukuta uharibifu mkubwa umekwishafanyika ikiwa ni pamoja na
duka la Mwenyekiti wa BAKWATA Wilaya ya Chato, Yusuph Idd, linalotumika
kwa biashara ya M-Pesa na vinywaji baridi likiwa linateketea kwa moto.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Ludorick Mpogolo, aliyefika eneo la tukio
muda mfupi baada ya polisi kuwasili, mbali na kusikitishwa na kitendo
hicho aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia
sahihi za kutatua mgogoro huo ambao unakua kwa kasi kila kukicha.
Hivi karibuni mgogoro huo wa kidini umezidi kukua wilayani humo kwa
pande hizo mbili kila upande ukidai ndiyo wenye haki ya kuchinja nyama
inayouzwa buchani
No comments:
Post a Comment