Kutokana na matokeo mabaya ya Mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwka jana, Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimetishia kufanya maandamano makubwa Nchini
kushinikiza waziri wa elimu Shukuru Kawambwa na naibu wake kujiuzuru ikiwa
hawatajiiuzuru kwa hiari ndani ya wiki mbili februari 19 mwaka huu
Bw. Mbowe amesema matokeo mabaya ya
Mitihani yanatokana na usimamizi mbovu wa viongozi husika katika wizara ya
elimu, na kwamba namna pekee ya kuwawajibisha ni kushinikiza wajiuzuru.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amelaani
vikali matukio ya uvunjifu wa amani
yanayotokana na Vurugu za kidini huku kikiyaita msiba kwa Taifa na adui mgeni
anayeathiri maendeleo ya wananchi huku
kikiwatahadharisha viongozi wake kujiepusha
na matukio hayo
Bw. Mbowe amesema Serikali imeshindwa kudhibiti matukio hayo
yanayoendelea kujitokeza hapa Nchini akitolea mfano matukio yaliyojitokeza hivi
karibuni ya Buseresere mkoani Geita na
huko Zanzibar ambapo Padre wa kanisa katoliki aliuawa kwa kupigwa risasi na
Kanisa kuchomwa moto
Aidha amesema viongozi wa CHADEMA watakaojihusisha na Vurugu
hizo hawatavumiliwa.
|
No comments:
Post a Comment