Wasfirishaji wa abiria kwapikipiki wakipata semina |
Bodaboda |
Watumiaji wa
vyombo vya moto hasa wapanda pikipiki wilayani Ngara mkoani Kagera wametakiwa kutii
sheria bila shuruti ili kuepusha mikwaruzano na vyombo vya dola nchini
wito huo
umetolewa na afisa polisi jamii wilayani ngara Bw. Respikiusi John wakati
akizungumza na wapanda pikipiki maarufu kama bodaboda katika mkutano wa wapanda
pikipiki uliofanyika leo katika ukumbi wa community center mjini ngara
Amsema kuwa
madereva wanatakiwa kuvaa kofia ngumu wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto
ili kuepuka kujitokeza kwa madhara pindi ajali inapokuwa imetokea.
“baadhi ya madereva pikipiki wamekuwa wakikiuka taratibu
kwa kutovaa kofia ngumu,kupakia abiria zaidi ya mmoja pamoja na kutokuwa na
kofia ya abiria wake hali hii ni hatari sana”
Aidha afisa
John amesema jesh la polisi halitokuwa na shida na dereva pindi anapokuwa
ametii sharia za usalama barabarani.
Katika
hatatua nyingine katika mkutano huo wapanda pikpiki hao wamechagua uongozi Bw. Lameck Kashula amechaguliwa kuwa
mwenyekiti Bw. Yasini Hassan akichaguliwa kuwa katibu wa umoja huo.
No comments:
Post a Comment