Na. Mwemezi Muhingo-KIBONDO
Vijana 571 operation sensa 2012 wa kikosi cha jeshi namba 824 wamemaliza mafunzo ya awali ya kijeshi katika kambi ya jkt Kanembwa wilayani kibondo mkoani kigoma wakiwa wamepata mafunzo mbali mbali ya kijeshi , uzalishaji , ufundi stadi , ujasiliamali pamoja na kutoa msaada wa shughuli mbali mbali za kijamii
Mgeni
lasmi katika sherehe hizo za kumaliza mafunzo ya awali kikosi 824 jkt
kanembwa alikuwa mkuu wa mkoa wa kigoma kanali mstaafu sahehe isa
machibiya na alianza kwa ukaguzi wa gwaride lililoandaliwa na vijana hao
Baada
ya ukaguzi huo vijana hao walikula kiapo mbele ya mgeni lasimi na
wageni mbali mbali walioambatana nae wakiwemo wakuu wa wilaya za mkoa wa
kigoma pamoja na viongozi wa kisiasa wageni waalikwa na viongozi wa kidini
Baada
ya zoezi hilo mkuu wa kikosi 824meja elasmos Bwegoge akitoa hotuba kwa
mgeni lasimi amesema kuwa jeshi la kujenga taifa linayo dira na dhima
katika kuwapokea na kuwafunza vijana kutoka sehemu mbali mbali bila
kujali kabila
Mjumbe
wa baraza la ngumi za lidhaa nchini BFT na mwakilishi wa wananwake
maendeleo ya vijana na ajila kwa wachezaji bi Zuena idd omary kipingu
amewataka vijana hao kuendeleza hishima na nidhamu waliyoipata katika
mafunzo yao
Nae
mkuu wa mkoa wa kigoma kanali mstaafu salehe issa machibiya ambaye
alikuwa mgeni lasmi katika sherehe hizo akitoa hotuba yake kwa wageni
waalikwa na vijana wanaomaliza mafunzo amewataka vijana kuwa na moyo wa kujituma na kujitolea ili waweze kulitumika taifa kwa moyo wote
Vijana
571 operation sensa 2012 wamemaliza mafunzo ya awaliya kijeshi katika
kambi ya jkt kanembwa ambapo wasichana walikuwa 105 na wavulana 466 na
vijana 9 wakishindwa kumaliza mafunzo hayo kutokana na sababu mbali
mbali
No comments:
Post a Comment