|
Mhashamu Baba Akofu Severin Niwemugizi wa jimbo Katoli la Rulenge Ngara akingia katika Kanisa la Mt. Francisco parokia ya Biharamulo kutoa daraja la Upadre kwa Shemasi Fortunatus Rweikiza |
|
Akimuombea kabla ya kumpadirisha |
|
Shemasi Fortunatus Rweikiza muda mfupi kabla ya kupadirishwa |
|
Askofu Niwemugizi akimwekea mikono kwaajili ya Baraka |
|
Mbele ya Shemasi Rweikiza muda mfupi kabla ya Kupadirishwa, Mapadre walimuombea. Anayeonekana hapo ni Padre Damas Missanga ambaye i Mkurugenzi wa Radio Kwizera |
|
Hapa ni baada ya kupadirishwa na kuvalishwa rasmi Mavasi ya Upadre |
|
baada ya Kupewa daraja la Upadre akaombea ili kuitenda kazi ya utume |
|
Askofu Niwemugizi akimpaka mafuta ya Krisma |
|
|
Askofu wa jimbo jilo Mhashamu severini Niwemugizi,Ijumaa ya
Julai 12,mwaka huu ametoa Daraja la Upadre kwa aliyekuwa shemasi Fortunatus
Rweikiza. Misa takatifu ya Upadirisho kwa Padre Fortunatus imefanyika katika
Kanisa Katoliki la Mt. Francisco parokia ya Biharamulo.
Aidha
katika hatua nyingine Askofu Niwemugizi ametoa wito kwa waumini wa Kanisa hilo
kujenga tabia ya kufunga ndoa na kuachana na dhana visingizio vya gharama
kwaajili ya harusi, na kuwataka wazazi kuhimiza watoto wao kufunga ndoa na
kukemea vikali visingizo vya mahari kwakuwa mambo hayo hayana uhusiano na
Kanisa
No comments:
Post a Comment