Mjumbe wa kamati tendaji ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wilayani Ngara Bw. John Simon Malanilo |
Mjumbe wa kamati tendaji ya chama
cha na maendeleo CHADEMA wilayani Ngara Bw Bw. John Simon Malanilo amesema kitendo cha serikali
kujichanganya kuhusu mpangilio wa madaraja kinaweza kuwachanganya watahiniwa wa
kidato cha nne ambao kwa sasa wanafanya mitihani yao ya kuhitimu elimu ya
sekondari nchini
Bw Malanilo ametoa kauli hiyo
alipozungumza na Radio Kwizera ya mjini
Ngara kuhusu kauli za maafisa wa juu wa wizara ya elimu nchini ambapo hivi
karibuni Katibu mkuu wa wizara hiyo Prof
Sifuni Mchome alitangaza kuwepo kwa daraja hadi la tano huku Naibu
Waziri Philip Mulugo akisema leo kuwa hakuna daraja la 5 badala yake litakuwepo
daraja la sifuri kama kawaida
Amesema kukinzana kwa viongozi hao
kunaonesha kutokuwa na mipango mizuri katika kuchochea maendeleo ya elimu
nchini na kwamba kinachoshusha ubora wa elimu nchini ni mipango isiyo madhubuti
katika wizara ya elimu
Aidha Bw Malanilo amesema malumbano
ya mpangilio wa madaraja kwa sasa hayana tija ambapo ameishauri serikali kuwekeza
katika kuwalipa walimu vizuri na kwa wakati, kuajiri walimu wa kutosha,
kuboresha vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kuboresha makazi ya walimu
Asante kwa ufafanuzi.Napenda kufahamu,huyu John Simon Malanilo ni ndugu yake na Peter Bujari?Na,je kwa jina jingine na yeye anaitwa John Bujari?Nitafurahi kama ndugu yangu mwandishi Juvenali nitapata majibu haya.Maana huyu jamaa kama vile namfahamu alikuwa Mwalimu wangu.Ni mtu makini sana japo nilikuwa bado mdogo,ila alikuwa na haiba ya uongozi na kufahamu mambo.NWAKILISHA
ReplyDelete