Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa,wananchi wakishiriki kufukua makaburi ya ndugu zao kupisha ujenzi huo.
Picha:- kwa hisani ya Dotto Jasson Bahemu na Simon Dionizy
Kijana ambaye jina lake halikufahamika mara moja akifukua kaburi |
wananchi wakitoa mabaki ya mwili wa marehemu katika kaburi kwenda kuyazika upya |
wananchi wakishuhudia zoezi la kuhamisha miili ya marehemu |
Zoezi la kuhamisha makaburi 40 kutoka katika eneo la ujenzi
wa kizuizi cha mpaka wa Tanzania na Burundi eneo la Nzaza kata ya Kabanga
wilayani Ngara Mkoani Kagera limefanyika November 04,2013.
Katika zoezi hilo mabaki ya milii ya marehemu imefukuliwa na
kuzikwa upya
Diwani wa kata ya Kabanga Bw Said Soud amesema kuwa zoezi
hilo limefanyika kwa amani
Bw Soud amesema kuwa wanafamilia wa Marehemu hao wameonyesha
ushirikiano wa kutosha, licha ya kuwepo
changamoto za matumizi ya vifaa duni vya
kufukua makabuli na kubeba mabaki ya miili ya marehemu
www.ngarakwetu.blogspot.com
imezungumza na baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambapo wengi wamesema serikali
imefanya jambo la maana kuwapatia fidia ya fedha za kuhamisha makaburi hayo na
kuzikwa upya kwa ndugu zao
No comments:
Post a Comment