Pichani ni mtoto mdogo kama anavyoonekana akishikilia Baiskeli wakati akimsubiri mama yake ambaye wakati napiga picha hii alikuwa akimtwisha nddo ya maji mwenzake,
Chanzo cha maji kikiwa kimefunikwa |
Kijana mdogo akichota maji na kuyajaza kwenye plastiki la lita 20
Pamoja na matumizi ya maji haya, ni sehemu pia ya watoto wanapochezea kama wanavyoonekana pichani
Ujenzi wa kuhifadhi chanzo hiki unaendelea. Ni hatari sana kwa watoto wadogo kuchezea maeneo hayo. kama picha inavyoonekana akiteleza kidogo lazima adodoke,ni hatari
Mwanablogu mwenzangu Bahat Anastars,ambaye ni Driver wa shirika lisilo la kiserikali CHEMA wilayani Biharamulo ambaye ndiye aliyewezesha usafiri kufika eneo hilo. Pichani anaonekana akitoa msaada kumtwisha ndoo ya maji mmoja wa mabinti waliofika kuchota maji.
NENO:- Mmoja wa wananchi waliozungumza nami katika eneo hili na kukataa jina lake nisiliandike amesema:-NI AIBU KWA TAIFA KAMA TANZANIA LENYE RASILIMALI NYINGI,UTAJIRI WA HALI YA JUU WATUWAKE KUNYWA MAJI KAMA HAYA .
No comments:
Post a Comment