Picha kutoka maktaba: Kulia mwenye kibaragashia kichwani(Juventus Juvenary) nikiwa na mzee Jovin Barahemana,Jovitho Jovin na wakazi wa Kijiji cha Mayenzi kata ya kibimba tukijadili masuala ya Ardhi |
Mkuu wa mkoa wa kagera kanal Fabian
Massawe amewataka wazee wenye malalamiko ya kuporwa ardhi na watu wenye uwezo
kifedha kupeleka malalamiko yao Serikalini ili wahusika wachukue hatua na wazee
wapate haki yao ya kumiliki Ardhi
Kanal Massawe amesema hayo kutokana
na malalamiko ya baadhi ya wazee
wilayani Biharamulo Mkoani Kagera kuomba serikali kuweka utaratibu
maalum wa kushughulikia migogoro ya ardhi inayowakabili wazee hao kwa madai kuwa
wananyanyaswa na watu wenye uwezo kifedha wanaovamia na kujimilikisha maeneo
yao
Wakizungumza na Radio Kwizera kwa
nyakati tofauti wilayani humo,Wazee hao wamesema kutokana na matendo hayo
wamejikuta katika hali ngumu kwakuwa hawana mtetezi
Mmoja wa wazee hao Domician Rwelamura mkazi wa kijiji cha Lukora
kata ya Runazi amesema kuwa zaidi ya hekari 3 za shamba lake zimevamiwa na mtu
mmoja ambaye hata hivyo amefanya naye kesi mahakamani kwa zaidi ya miaka 2 na bado
haki haijapatikana
Kutokana na Malalamiko hayo Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Kanal Fabiani Massawe ameziagiza mamlaka husika kuhakikisha
wanatumia vizuri nafasi zao kutatua migogoro hiyo na kuwachukulia hatua watu
wanaotumia uwezo wao kifedha kupora ardhi na kuwanyima haki wazee. EndS
Mzee Domician Rwelamura,mkazi wa Lukora Biharamulo akizungumza nami namna alivyoporwa ardhi na kigogo mwenye pesa |
Akionesha nyaraka na vielelezo |
No comments:
Post a Comment