July 11, 2014

WEKENI AKIBA YA CHAKULA,MAZAO YA CHAKULA YASIPIKWE POMBE

Ni kauli ambayo mara kwa mara na kwa nyakati tofauti imekuwa ikirudiwa na viongozi mbali mbali kama hamasa ya wananachi kutunza akiba ya Chakula ili kuepuka njaa.

Ka mara ya Mwisho nakumbuka kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Biharamulo Bw.Lichard Mbeho wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Nyarubungo kijiji cha Katoke wakati wa maadhimisho ya siku ya SERIKALI ZA MITAA.

Leo :- Niko katika kijiji kimoja wilayani Ngara Mkoa wa Kagera. kinachoonekana hapa ni mtambo wa kutengenezea Pombe ya Moshi(Gongo). Pombe yenye majina mengi.....Kalinya,Waragi,Gongo,White,na mengine mengi kulingana na wenyeji wa maeneo husika.

Bila kutaja majina na kutowekwa picha za wahusika katika Blogu hii, nimeelezwa kuwa hii ndiyo kazi kwa miaka mingi na chanzo cha Mapato kwaajili ya shughuli zao za kila siku na MAISHA YANASONGA!!!!



Pichani , ni Mimi Juventus Juvenary katika utafiti wangu na Uchunguzi juu ya GONGO INAVYOTENGENEZWA.
Ni ukweli usiopingika kuwa matumizi ya Pombe hii yana madhara!!  nimeshuhudia watumiaji wa kupitiliza wa Pombe hii wakiathirika kutokana na UKALI wa pombe hii hali inayopelekea kuchoka kwa mwili na kuwa wadhaifu sana kiasi cha kushindwa kufanya kazi.

Vijijini pombe hii inapendwa sana,lakini inawaathiri pia kutokana na matumizi yake wakati LISHE NI DUNI!.                       katika mazungumzo yasiyo rasmi jamaa mmoja ameniambia kuwa Pombe hii ndio iliyomsomesha kwakuwa wazazi wake walikuwa wakitengeneza na kuuza hatimae kupata fedha zilizomsomesha sasa ni mkubwa serikalini!!!!!!!! KITU KINACHOITWA POMBE HARAMU,KIMEKUWA HALALI KWA UPANDE MWINGINE!!!!!!! anasema" Bora serikali ingehalalisha na kuifanya kuwa Pombe rasmi kama zilivyo nyingine ikiwezekana Serikali ipate mapato kutokana na Kodi" sitaki kuwa msemaji sana wa hili.....

UJUMBE:-WEKENI AKIBA YA CHAKULA,MAZAO YA CHAKULA YASIPIKWE POMBE
 Kauli hii imeonekana kupuuzwa kutokana na kuwa Mazao mengi hasa Mahindi na Ndizi hutumika kupikia gongo hali inayoashiria kuendelea kuzalishwa/kutengenezwa ka pombe hii kila siku na Mazao kuisha ikiwa jitihada za kilimo hazitatiliwa mkazo.

kwa mawazo,maoni,mchango na lolote lile kuhusiana na hiii, tafadhali niandikie........juventusjuvenary@gmail.com au nipigie simu 0756432748

No comments:

Post a Comment