Fredrick Manyanda |
Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili imetangaza ratiba ya kwanza ya ziara yake katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Mbeya inayoanza Septemba 17, hadi Oktoba 6, mwaka huu.
Ziara hiyo inayolenga kukusanya taarifa na kupokea malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili inaanza katika mkoa wa Kigoma ambako itakuwapo huko kwa muda wa siku nane (Kigoma Septemba 17, Kibondo Septemba 18, na Septemba 19, Kasulu Septemba 20 na 22 na Uvinza Septemba 23 na 24).
Kwa mujibu wa Taarifa ya Tume hiyo iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Tume Fredrick Manyanda, tume itakuwa katika mikoa ya Rukwa na Katavi kuanzia Septemba 25 hadi 30.
Alisema, Septemba 25 hadi 27, tume itakuwa Mpanda na Septemba 28 hadi 30, itakuwa mjini Sumbawanga.
Aidha Tume itakuwa katika mkoa wa Mbeya ambapo itatembelea katika wilaya za Mbozi, Mbeya na Mbarali kuanzia Oktoba Mosi hadi 6.
Itakuwa katika wilaya ya Mbozi Oktoba Mosi na 2, Mbeya mjini Oktoba 3, na itamalizia ziara yake katika wilaya ya Mbarali Oktoba 5 na 6.
Aidha pamoja na ziara hiyo, Manyanda amesema tume inaendelea kupokea taarifa na malalamiko kwa njia ya barua, simu na barua pepe
No comments:
Post a Comment