Source:DW ......Mpiganaji ngumi nyota kutoka Ufilipino Manny Pacquiao amepuuzia majigambo ya Floyd mayweather , akisema anamuonea huruma hasimu wake huyo Mmarekani na anamtaka kusoma biblia.
Mpiganaji ngumi nyota kutoka Ufilipino Manny Pacquiao amepuuzia
majigambo ya Floyd mayweather , akisema anamuonea huruma hasimu wake
huyo Mmarekani na anamtaka kusoma biblia.
Katika vituko vya hivi karibuni, Mayweather , ambaye hajawahi kushindwa katika mapambano yake 47, ameweka picha kadhaa katika mtandao wa kijamii , akimuonesha Pacquiao akiwa ameangushwa chini katika mapambano yaliyopita. Ameongeza kuwa Pac Man amechacha hana kitu mfukoni anasubiri malipo.
No comments:
Post a Comment