June 2, 2015

KAULI MBIU:-VIJANA KAZI,WAZEE USHAURI

Ni kauli inayotumika kwa sasa hasa inatumiwa na Vijana waliotangaza nia ya kugombea nafasi mbali mbali za uongozi hasa Udiwani na Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.


1.Juventus Juvenary Illambona

Juventus Juvenary

 Mawasiliano .....0756432748
Ni Kijana mwenye umri wa miaka 34. Mzaliwa wa kijiji cha Buhororo kata ya Kibimba wilayani Ngara katika Mkoa  wa Kagera. Darasa la 1-7 alisoma katika Shuke ya Msingi Buhororo. Kidato cha kwanza alisoma katika shule ya sekondari ya ufundi Kage(Kange Technical Secondary School ) iliyopo Jijini Tanga. Baadae alihamia katika shule ya sekondari Wailes iliyopo Temeke jijini Dar es salaam kidato cha pili hadi cha nne.
Kitaaluma ni mwana habari ,taaluma aliyoisomea katika chuo cha uandishi wa Habari Royal College of Tanzania RCT, zamani kilifahamika kama RCJ Royal College of Journalism. Ni Mtia nia katika ngazi ya Udiwani. Anagombea udiwani katika kata ya Kibimba nafasi ambayo kwasasa inashikiliwa na Mh.John Shimilmana ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri kwasasa. Ni kazi ngumu na kubwa kupambana na kigogo. anawaomba wote wanaomuunga mkono kumchangia mawazo na rasilimali hasa fedha na vifaa vya hamasa ili kufanikisha nia yake kwa maendeleo ya wana Kibimba,Ngara na Taifa kwa ujumla.

2.MARWA JOHANES MARATO

Marwa Johanes Marato

 Mawasiliano....0763312267
Huyu pia ni kijana kutoka jimbo la Butiama kata ya Sirorisimba Mkoani Mara. Ni kijana machachari na mwenye uwezo na uzoefu mkubwa Kisiasa. Kitaaluma ana shahada ya uzamili(Masters) katika masuala ya afya ya umma.

Katika Uchaguzi mkuu 2015 ametia nia kugombea ubunge jimbo la Butiama ambalo kwasasa linaongozwa na Mh.Nimroad Mkono ambaye ni miongoni mwa wabunge matajiri japo mpinzani wake kisiasa anasema ni jimbo masikini sana likilinganishwa na rasilimali zilizopo hasa madini na Mto Mara ambao kama ungetumika vizuri ungeweza kuleta tija katika kilimo cha Umwagiliaji.

Ni kijana ambaye ni mzalendo,aliyezaliwa na kukulia katika familia ya wakulima na wafugaji. Kutokana na sifa hiyo yeye mwenyewe anasema anazifahamu changamoto zinazoikabili jamii ya wafugaji na wakulima kutokana na kuwa yeye ni sehemu yao.
Vijana wote hao wawili Juventus Juvenary Mgombea udiwani, na Marwa Johanes Marato wanaingia katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.

No comments:

Post a Comment