Kwa muda mrefu wahudumu wa afya ya
masuala ya ngono wamesisitiza matumizi ya mipira ya kondomu kama mbinu
bora zaidi dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Lakini tabia moja hatari ya kutumia madawa ya kulevya na wapenzi wa jinsia moja inazidi kuibua wasiwasi.kumekuwa na njia nyingi za kinga dhidi ya virusi vya ukimwi, lakini kuna dawa moja mpya - Pre-Exposure Prophylaxis (PrEP) - ambayo inaweza kutoa kinga dhidi ya maambukizi ya ukimwi iwapo itatumika kabla ya kushiriki ngono.
Utafiti unaofanywa na daktari Sheena McCormack kutoka chuo kikuu cha London, unasema kwamba unapomeza dawa hiyo, inazuia maambukizi ya ukimwi kwa kuzuia ongezeko la virusi, hii ni baada ya majaribio kufanyiwa kundi moja la wapenzi wa jinsia moja, ambao wamo katika hatari kubwa zaidi ya maambukizi
Shirika la afya duniani limetambua kwamba dawa hiyo ya tembe inaweza kupunguza maambukizi kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa dawa ya aina hii inahamasisha watu wengi kushiriki ngono bila kutumia mipira ya kondomu
Hata hivyo matumizi ya dawa hii haizuii maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na kaswende, je, kukubalika kwa matumizi ya dawa hii duniani kunamaanisha ongezeko la magonjwa ya zinaa.
................................................................................................................................................................
kwa msaada wa mtandao wa - http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/07/150704_hiv-aids
No comments:
Post a Comment