www.ngarakwetu.blogspot.com iko mjini Kahama katika Soko la wakulima,hali inayoonekana hapa ni kukithiri kwa uchafu!!!!!!!! hali inayohatarisha maisha ya watumiaji. Juventus Juvenary kama mwanahabari anayefanya kazi na Radio Kwizera ameandika habari.
KAHAMA
Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya
Mji wa Kahama mkoani Shinyanga wanaotegemea huduma kutoka katika Soko la
wakulima Mjini Kahama wameeleza kuwa hali zao kiafya ziko mashakani kutokana na
kukithiri kwa uchafu
Hayo yameelezwa na wananchi hao
wakati wakizungumza na Radio Kwizera sokoni hapo
Mmoja wa wafanya biashara wa Mboga za majani katika
soko hilo Bi.Paskazia Elias amesema hali ya uchafu wa soko hilo unahatarisha
maisha yao,huku mfanya biashara wa kuku Bw.Adidas Gideon akiitaka Srikali kuongeza
hamasa kwa uongozi wa soko kuhusu usafi
Insert:-wafanya Biashara
Kutokana na hali hiyo,Afisa afya wa
mji wa Kahama Bw.Deogratis Simon Dotto ametoa wito kwa wafanya Biashara sokoni
humo kuzingatia masharti ya afya kwa kufanya usafi huku akisema kuwa watakaokiuka
watachukuliwa hatua. EndS
|
Juventus Juvenary akizungumza na mmoja wawafanyabiashara katika soko la wakulima mjini Kahama Bi Paschazia Elias |
|
Kutoka kushoto ni Mwanahabari Simon Dionizy akirekodi sauti ya mfanya biashara,aliyesimama ni Juventus Juvenary-ngarakwetu.blogspot.com |
|
Uchafu sokoni |
|
Juventus |
|
Juventus akielekea Sokoni |
|
Simon Dionizy akifanya mahojiano na mfanya Biashara sokoni kuhusu hali ya usafi |
Hali ni ya hatari! Jitihada za maksudi zinatakiwa kuchukuliwa ili kunusuru afya za wananchi.
|
mahojiano na wafanya biashara wengine |
|
Mawe kwaajili ya ujenzi wa miundombinu sokoni |
|
Moja ya maduka ya nyama sokoni hapo. Idara ya Afya Katika Halmashauri ya mji imetoa notisi ya siku 90 kwa wamiliki wa maduka hayo kuhakikisha wanaboresha huduma kuepuka kufungiwa |
Picha na Emmanuel Mlelekwa-ngarakwetu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment