Rais wa baraza la Maaskofu wa
Kanisa Katoliki Tanzania Mhashamu Askofu Taracisis Ngaralekumtwa amewataka
waumini wa Jimbo Katoliki kahama kumuenzi aliyekuwa Muasisi wa jimbo hilo kwakufanya
kazi kwa bidii na kuimarisha mshikamano
Askofu Ngaralekumtwa ametoa rai
hiyo wakati wa Ibaada ya mazishi ya hayati Askofu Matheo Shija aliyefariki
dunia Disemba 9 mwaka huu baada ya kuanguka ghafla mbele ya nyumba aliyokuwa
akiishi
Katika ibaada hiyo iliyofanyika
kwenye kanisa kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga mjini Kahama,rais huyo wa Baraza
la Maaskofu wa Katoliki amesema Hayati Askofu Matheo Shija alikuwa na mchango
mkubwa katika kanisa kwa kuziishi TUNU zilizolenga kuendelea mshikamano Nchini
Akitoa salaam za rambi rambi kutoka
Kwa kiongozi wa dhehebu la Kikatoliki Duniani Papa Francis katika Ujumbe wake
uliowasilishwa na Barozi wake hapa NchiniAskofu Mkuu Francisco Pardilla amesema
baba Mtakatifu anaungana na waumini wa Jimbo la Kahama katika kipindi hiki cha
huzuni na kuwataka kuenzi matendo mema aliyoyaasisi.
Mazishi ya askofu Shija
yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kidini,Vyama na Serikali kutoka sehemu
mbali mbali, ambapo katika salaam za rambi rambi kutoka baraza la Maaskofu wa
Katoliki zilizowasilishwa na rais wa Baraza hilo Mhashamu Askofu Taracisis
Ngaralekumtwa amewataka waumini wa Jimbo Katoliki kahama kumuenzi askofu
Shija kwakufanya kazi kwa bidii na
kuimarisha mshikamano
Naye Balozi wa Papa hapa Nchini Askofu
Mkuu Franchesco Pardilla kakatoa salaam
za rambi rambi zikiambatana na ujumbe kutoka kwa kiongozi Mkuu wa Kanisa
Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Papa Francis
Awali ilitegemewa kuwa Rais wa
jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli angeshiriki katika maziko
hayo,lakini taarifa zilizotolewa na mmoja wa wasemaji zikaeleza kuwa ametoa
taarifa za kutofanikiwa huku akiwatakia Pole waumini ndugu jamaa na Viongozi wa
dini
Licha ya sifa kemkem zilizotolewa
kwa hayati Askofu Shijja,Mkuu wa wilaya ya kahama Vitta Kawawa akamtaja kuwa
alikuwa kiungo kikubwa kufanikisha maendeleo na ustawi wa wilaya hiyo,na
mchango mkubwa kwa Serikali kutokana na kuwa alikuwa akiwasaidia wafungwa kwa
huduma mbali mbali
No comments:
Post a Comment