Wilaya ya Kahama iliyoko Mkoani Shinyanga,imetajwa kuwa na Kiwango kikubwa cha Ukatili wa Kijinsia hasa kwa watoto
kunyanyaswa,watoto wa Kike kubebeshwa Mimba na wanawake kubakwa na kupigwa
Mkurugenzi wa Miradi ya SHDEPHA Kahama,Bw.Venance Muzuka akizungumza na Vyombo vya habari |
Bw.Mzuka amesema kwa watoto pekee
Jumla ya watoto wa kike 21 katika shule mbalimbali za Sekondari katika Halmashauri
ya mji wa Kahama wameripotiwa kubebeshwa mimba katika kipindi cha January hadi
September mwaka huu
Mkurugenzi wa SHDEPHA Bw.Venance Muzuka(Kulia,) akizungumza na Vyombo vya habari, pembeni yake ni Bw.Kazungu Barnabas ambaye ni Msimamizi wa msimamiizi/anayeshughulikia masuala ya Wahanga wa ukatili |
Aidha mkurugenzi huyo amesema Shirika
lake linatarajia kufanya maadhimisho ya ukatili wa kijinsia kuanzia Novemba 25
hadi Decemba 10 mwaka huu ambapo Katika kipindi hicho cha maadhimisho, wito
umetolewa kwa wananchi wote hasa waliowahi kufanyiwa ukatili kujitokeza
kwaajili ya kupatiwa huduma za upimaji wa afya, Ushauri wa kisheria na
Saikolojia.
Kushoto ni Bi.Shekha Nassor ambaye ni Mratibu wa Mradi wa SAUTI ulioko chini ya SHDEPHA akiwa na Muelimishaji rika Bi.Edith Edward Mugerezi |
Mkurugenzi wa SHDEPHA Bw.Venance Muzuka na Bi.Shekha Nassor ambaye ni Mratibu wa Mradi wa SAUTI |
Naye, Muelimishaji rika wa shirika hilo Bi.Edith Edward
Mugerezi amesema vitendo vya ykatili wa kijinsia vinaiweka jamii katika uduni
wa maendeleo kwakuwa wahanga wengi huathirka kisaikolojia na wengine kupata
maambukizi ya virusi vya UKIMWI. EndS
www.ngarakwetu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment