Hii ndio Ngara. na watu wa kuoikomboa Ngara ni mimi na wewe!
Siku ya leo ngarakwetoblog imekutana uso kwa uso na mtaalam
wa Kilimo na Mifugo Jonas Kizima. Kwa asili ni mzaliwa wa Kijiji cha Buhororo
Ngara, kwa sasa yuko Chuo kikuu cha Sokoine Morogoro, ambaye katika safu hii
anakuja na somo:-
___________________________________________________
Sekta ya mifugo kama zilivyo shghuli nyingine za kibinadamu
za uzalishaji mali za, ni miongoni mwa sekta zenye kuhusika katika uharibifu wa
mazingira kama shughuli hizo hazijawekewa mikakati na jamii au mamlaka
husika. Lakini pia mbali na uharibifu wa
mazingira pia sekta ya mifugo pamoja na watumiaji wengine ardhi huweza kusababisha migongano ya matumizi ya rasilimali
Mifugo imekuwa ikinyooshewa vidole na sekta
nyingine Mfano mamlaka za barabara kuharibu kingo za barabara. Kwani mfumo wetu
wa ufugaji haujaweza kutengenisha au kuainisha rasmi mgawanyo au mpango wa
matumizi bora ya ardh ili kila sekta iweze kuwa na mifumo yake ili KUEPUSHA
MIGGOGORO , kutokana na uharibifu wa mali au uvunjifu wa amani katika jamii
|
Katika Picha. Mtaalam(Mtafiti) Jonas B.Kizima kutoka Chuo Kikuu Sokoine akipima nyasi kwa kipimo maalumu. ni katika Jitihada za kuboresha marisho ya Mifugo |
Katika picha hapo juu linaonekana kundi la Ng'ombe wakipelekwa malishoni
|
Taswira ya Rusumo |
Baadhi ya maeneo ya Rusumo kwenye vilima/miteremko
yanayoonesha dalili za uharibifu wa mazingira unaoweza kuleteteleza mmomonyoko
wa ardhi kutokana na mifugo kuyatumia maeneo ya malisho kupita kiasi. Bado upo
umuhimu wa wataaalamu kupima na kuainisha uwezo wa eneo la malisho kujua ni
mifugo mingapi inaweza kulishwa eneo hilo, ili kutoa ushauri kwa wafygaji na wadau wengine ili kuongeza uzalishaji wa
mazao ya mifugo na kuepusha uharibifu wa nyanda za malisho ( overgrazing)
|
Timu ya wataalam ikipata maelezo kutoka kwa meneja wa REDESO Ngara Bw. Leonce Batondana |
Jitihada mbalimbali za mashirika zimekuwepo wilayani
Ngara kusaidia kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji, hapa mtaaalamu ( Meneja
wa shirika la REDESO ndugu Leons BATONDANA akitoa maelezo kwa wageni kuhusu
jitihada za shirika lake kwa kusaidiana na mashirika mengine kuzalisha miche ya
MITI ya ASILI ipatikanayo kweneye vyanzo vya maji ili iweze kupandwa katika
vyanzo vya maji ( water catchment
|
Kulia katika Picha ni Ndg. Leonce Batondana, Meneja wa mradi REDESO akitoa maelezo katika moja ya vitalu vya kuoteshea miche ya miti |
|
Shamba darasa |
|
Kilimo Mseto |
|
Shamba linapendeza |
www. ngarakwetu.blogspot inapenda kukushukuru ndugu Jonas B. Kizima, mtaalam wa mifugo na Kilimo. tunatambua mchango wako na tunaamini kwa jitihada zako sekta ya mifugo na kilimo itawanufaisha wananchi wa Ngara na kuwakwamua Kimaisha. nasi tunaahidi ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha dhamira ya dhati ya maendeleo inatimilizika
No comments:
Post a Comment