October 4, 2013

WAZIRI SAMWELI SITTA WA AFRIKA MASHARIKI AFANYA ZIARA NGARA

Waziri Samweli Sitta akiwa katika jumba la mapokezi la Viongozi (Ikulu ndogo),Mjini Ngara

Kushoto ni naibu Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda Bw. Francis Mwaipaja

Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw.Costantine Kanyasu akitoa Taarifa ya wilaya kwa Waziri Sitta

Waziri Sitta na Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu wakibadilishana mawazo katika Kivuko cha Mto Ruvubu,kuelekea Rusumo Mpakani mwa Tanzania na rwanda

Wakivuka



Akisalimiana na wakandarasi kutoka Japan wanaojenga kituo cha forodha upande wa  Tanzania na Daraja linalunganisha Tanzania na Rwanda

Waziri Sitta akitoa hotuba

Akipewa taarifa ya maendeleo ya Mradi.


Daraja




Akizungumza na wanafunzi wa Rusumo Sekondari

Ofisi mpya Idara ya uhamiaji,Polis na TRA baada ya majengo ya awali kubomolewa kupisha upanuzi





Picha zote na Maelezo ni kwa hisani ya mwanahabari wetu Shaaban Ndyamukama-Ngara


Wito umetolewa kwa wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera kutumia fursa zinazopatikana kupitia miradi mitatu ya Rusumo wilayani humo kuhakikisha wanajiinua kiuchumi  kwa kufanya biashara baina yao na wenzao kutoka  jirani.

Waziri wa Afrika ya mashariki wa Tanzania Bw. Samweli Sitta amesema hayo leo wilayani Ngara wakati akiongea na wakazi wa rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda katika ziara yake ya kutembelea mipaka ya wizara yake

Bw Sitta amesema miradi ya Rusumo ya ujenzi wa umeme kituo cha forodha na daraja kati tya Rwanda na Tanzania ni viungo katika kuimarisha mahusiano mema ya kiuchumi kwa kufanya biashara ya kuuziana bidhaa mbalimbali

Hata hivyo amewahakikishia wakazi wa Rusumo kuwa changamoto zinazowakabili wananchi wa eneo hilo hasa maji umeme na makazi bora ya watumishi yatafikishwa serikalini  ili kuhakikisha wanaishi  katika mazingira rafiki.

 

 

 

No comments:

Post a Comment