November 22, 2013

MAJAMBAZI YA PORA NA KUJERUHI BIHARAMULO. JESHI LA POLISI LAAPA KUYASAKA


Zaidi ya watu 10 wanasaidkiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za kivita(Bunduki aina ya smg) wameteka magari 15 na kupora vitu mbalimbali zikiwemo fedha ambazo thamani yake haijafahamika na kuwa jeruhi  baadhi ya watu  wilayani Biharamulo Mkoani Kagera
IGP Said Mwema(Pichaya maktaba)
Mmoja wa majeruhi ambaye amelzwa katika Hospitali teule  ya wilaya ya Biharamulo Bw.Gideon Chango amesema tukio hilo limetokea  Novemba 21 majira ya saa 10 jioni katika kijiji cha Busiri kata ya Lusahunga, wakati wakielekea katika mnada wa Ng'ombe.

Kaimu Kamnda wa Polisi Mkoa wa Kagera Henry Mwapati amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba msako mkali unaendelea dhidi ya majambazi hayo yaliyokimbilia porini baada ya uharifu huo

No comments:

Post a Comment