Mkuu wa wilaya ya Biharamulo Bw. Richard Mbeho |
Wahitimu |
Mkuu wa wilaya akiwa na Mkuu wa Seminari ndogo ya Katoke |
Wanafunzi wa katoke seminari |
Mapadre, katika Misa takatifu kama sehemu ya mahafali |
Na Shaaban Ndyamukama November 17, 2013
BIHARAMULO: Wahitimu
wa ngazi mbalimbali za elimuwametakiwa kutumia maadili waliyopata katika shule
zao kulinda Amani na kuleta maendeleo kwa kutumia taaluma zao ikiwa ni pamoja na kujiendeleza
kuongeza ujuzi na maarifa.
Mkuu wa
wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Bw Richard Mbeho ametoa wito huo Nov 16
katika mahafali ya 40 ya wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya seminari ya
katoke inayomilikiwa na jimbo katoliki
la Rulenge mkoani Kagera.
Bw Mbeho amesema
kuwa pamoja na kutumia taaluma mbalimbali hawana budi kuwa makini na utandawazi
kwenye mazingira yao kwani unaweza
kuchangia kujiingiza katika vitendo viovu na kuhatarisha usalama wa maisha yao.
“Jiepushe na
rushwa kwa kutaka mali, madaraka,ngono
na hatimaye kujiingiza kwenye vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalamana Amani
kupitia njia za utandawazi”.Alisema Mbeho
Amewahimiza
na wahitimu kujiendeleza kitaaluma na wazazi kuendelea kutoa malezi kwa watoto wao ili waendelee kutegemewa na taifa kwa kutoa
huduma mbalimbali ndani ya jamii zao.
Awali katika
ibada ya misa kwa wahitimu hao mkuu wa shule ya seminari ya katoke padre Frolian
Tuombe amesema shule hiyo inatoa masomo yote yakiwemo ya ya kiroho kwa kulinda maadili i kwa nadharia
na vitendo
Padri Tuombe
amewataka wahitimu kufanya kazi kwa uadilifu kwa mujibu wa Imani yao kwa
kuzingatia utii wa sheria kanuni za utumishi na kuwajibika bila kwa kulinda
haki pasipo kuwa na uonevu wala ubaguzi wa aina yoyote
Katika
mahafali hayo zaidi ya Tsh mil 2.59/- zimechangwa na wazazi wa wanafunzi waliohitimu
kidatocha nne mwaka huu katika shule hiyo
ambapo fedha taslimu ni Tsh 775,200 ili kupunguza
changamoto mbalimbali zinazoikabili jumuia ya shule.
No comments:
Post a Comment