Na Anord Kailembo-www.ngarakwetu.blogspot.com
Katika uchaguzi wa kura za maoni wilayani Ngara wa
kumpata mgombea ubunge wa kuwakilisha chama cha mapinduzi CCM ulikuwa kama
ifuatavyo
Watangaza nia ya kugombea ubunge
kupitia chama hicho ni 9 ambao ni Alex Gashaza,Elena Gozi,Issa Sama,Dr Filimon
Sengati,Jerard Muhile,Sprian Muhelanyi,Radslaus Bambazi,wilidard Ntamalengero
na Johakimu Nchunda.
Wanachama waliotarajiwa kushiriki
katika uchaguzi huo ni 50,717
Walioshiriki uchaguzi ni 32,589
Kura zilizoharibika ni 566
Walioshiriki ni 32,028
MATOKEO NI KAMA ITUATAVYO:
MAJINA
KURA ASLIMIA
1:Alex Gashaza I0,814 33.7%
2:Issa Samma 7,167 22.38%
3:Ellena Gozi 5,474 17.09%
4:Dr.Filimon Sengati 4,393 13.72%
5:Jerad Muhile 1,866 5.83%
6:Spirian Muhelanyi 927 2.89%
7:Ladislaus Bambazi 636 1.99%
8:Wilbard Ntamalengelo 390 1.22
9:Johakimu Nchunda 357 1.11
Katibu wa chama hicho wilayani
Ngara Bw.Jacob Makune amesema kuwa waliokuwa wakichuana kuwania nafasi ya
ubunge kupitia chama hicho waungane kwa pamoja kuhakikisha wanashirikiana na
Bw.Gashaza ili mbunge wa jimbo la Ngara
aweze kutokana na chama hicho.
Nao wanachama wa chama hicho
walioshiriki uchaguzi huo wamesema kuwa changamoto iliojitokeza ni pamoja na
kucheleweshwa kwa vifaa vya kupigia kura katika baadhi ya maeneo hali
iliyopelekea wanachama wengine kushindwa kupiga kura.
No comments:
Post a Comment