Barack Obama amempokea mrithi wake Donald Trump katika Ikulu ya White House, Novemba 10, 2016. |
Barack Obama amempokea Donald Trump katika Ikulu ya Marekani ya White Hoiuse Alhamisi hii. Mkutano rasmi ili kuanza kipindi cha "mpito chenye mafanikio" uliyopendekezwa na Rais wa sasa wa Marekani.
Barack Obama na Donald Trump hawakuficha tafauti zao wakati wa kampeni, Barack Obama hakusita kumuita Donald Trump "tishio kwa Marekani." Lakini sasa, rais anayemaliza muda wake amekutana kwa mazungmzo na mrithi wake.
Donald Trump aliwasili mjini Washington katika ndege yake binafsi, kabla ya gari kumpeleka Ikulu ya Marekani ya White House.
Siku ya Jumatano Barack Obama aliwataka Wamarekani kumheshimu rais aliyechaguliwa na taasisi mpya. Donald Trump, katika hotuba yake ya ushindi alionekana akiongea kauli yenye busara, ikilinganisgwa na hapoa awali wakati wa kampeni zake, mwandishi wetu mjini Washington, Anne-Marie Capomaccio amearifu.
"Mazungumzo mazuri"
Baada ya mkutano wao, Barack Obama na Donald Trump kwa kipindi cha dakika chache walionekana wakitabasamu mbele ya kamera baada ya saa moja na nusu ya mazungumzo ambayo waliyataja kuwa mazuri na yenye kujenga. Rais anayemaliza muda wake hata hivyo amebaini kwamba 'mazungumzo yalikua mazuri'. Ameahidi kufanya "kiliyo chini ya uwezo wake" kwa mafanikio ya Donald Trump. Kauli kama hiyo ilitolewa na Donald Trump, ambaye amesema "yuko tayari kufanya kazi na rais," anayemaliza muda wake.
Mapema kikosi cha kampeni ya Trump kilikutana na washauri kujadili masuala kuhusu siku za kwanza 100 za Trump kama rais na uteuzi muhimu katika nyadhifa za serikali.
Mkutano huu ulikua pia fursa kwa wake wa wanasiasa hawa wawili kukutana kwa mazungumzo.
Trump anatarajiwa kuapishwa tarehe 20 mwezi Januari mwakani, na kuwa rais wa 45 wa taifa hilo lenye nguvu duniani baada ya kuibuka mshindi wa uchaguzi wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment