April 3, 2016

BOB MARLEY-Atakumbukwa kwa mengi.

Aliwahi kusema, "Wananiita chotara,lakini mimi siegamii upande wowote bali nipo upande wa Mungu aliye niumba kutoka kwa weusi na weupe".

Alikataa kuandika urithi kwa kuamini kuwa marastafari huwa hawafi
Robert Nesta Marley,ambaye baadaye alikuja kujulikana kama Bob Marley,alizaliwa Februari 6,1945 katika kijiji cha Nine Mile kwenye Parishi ya mtakatifu Ann huko Jamaica.Baba yake Norval Sinclair Marley alikuwa mzungu na mama yake Cedelia Booker alikuwa Mjamaica mweusi.







Historia ya maisha yake haitofautiani sana na wanamuziki wenzake wa reggae Peter Tosh aliyelelewa na shangazi yake na Bunny Wailer aliyelelewa na baba yake zaidi,ni historia ya huzuni iliyo muacha Bob Marley chini ya mzazi mmoja(mama yake) pale alipofiwa na baba yake akiwa na umri wa miaka kumi tu.Norval Sinclair (baba yake Bob Marley) alikuwa nahodha wa meli na muangalizi wa mashamba,alikufa mwak 1955 akiwa safarini,wakati huo alikuwa na umri wa miaka 60.

 
Mbali na Muziki wa Reggae,Bob Marley pia alikuwa mpenzi wa Mchezo wa Mpira wa Miguu

Kifo hicho kilimfanya mama yake Bob Markey ahamishe makazi kwenye mji wa Kingston,huko Bob alikutana na Bunny Wailer wakawa marafiki na kujifunza muziki pamoja.Akiwa na umri wa miaka 14,Bob Marley aliacha shule na kujiunga na chuo cha ufundi wa kuchomelea vyuma,muda wa kewa kupumzika alikuwa na Bunny Wailer kwenye muziki,kipindi hicho mwalimu wao alikuwa Joe Higgs,muimbaji wa mtaani mwenye imani ya kirastafari.
Chini ya Joe Higgs walikutana na Peter Tosh na kuungana naye.
Mwaka 1962 Bob Marley alirekodinyimbo zake mbili za kwanza ambazo ni;"Usihukumu"(judge not) na "kikombe kimoja cha chai"(one cup of tea) chini ya muandaaji Leslie Kong,lakini nyimbo hizo hazikukubalika sana.Mwaka 1963 akashirikiana na Bunny Wailer,Peter Macintosh(Peter Tosh),Junior Braithwaite,Beverly Kelso na cherry Smith na kuunda kundi la "The Teenagers" kundi hilo lilijibadili majina na kuwa "The wailing rude boys","The wailling wailers" na mwishowe "The wailers".
Mwaka 1964 na 1965 watoa vibao vikali kama "Usiwe na wasiwasi"(simmer down) na "Nafsi isiyokubali"(soul rebel)nyimbo hizi zilikonga nyoyo za Wajamaika wengi. Hata hivyo kufikia mwaka 1965 lilibakiwa na wakali watatu tu,yaani Bob Marley,Bunny Wailer na Peter Tosh,baada ya wengine kujiengua.

Mwaka 1966 Bob Marley alimuoa kimwana Rita Anderson na kwenda kuishi kwa muda na mama yake huko Wilmington,Delaware nchini Marekani na kuibuka na imani kali ya kirastafari na kuja na mtindo wa kufuga nywele uitwao "dreadlocks". Baada ya hapo Bob Marley na kundi lake la The wailers walitoa vibao kemkem vilivyoitikisa Dunia.Kati ya vibao hivyo ni;Africa unit,Zimbabwe,Could oyu loved?,Iron lion zion,Is this love,Buffalo soldier na vingine vingi.Huyo ni Bob Marley,mfalme wa reggae aliyepinga ubaguzi kwani hata yeye mwenyewe alisema "Wananiita chotara,lakini mimi siegamii upande wowote bali nipo upande wa Mungu aliye niumba kutoka kwa weusi na weupe".
Gari alilokuwa akilitumimia hadi mauti yanamkuta. Kwasasa limeegeshwa katika Makumbusho huko Kingston-Jamaica



No comments:

Post a Comment