Na,Juventus
Juvenary-Ngara
Kundi la
watu wanaosadikiwa kuwa majambazi limemvamia mfanyabiashara katika kijiji cha
Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera na kumpora fedha kiasi cha shilingi laki
nane
Tukio hilo
limetokea Alhamisi Disemba 5 mwaka huu majira ya saa 4 usiku,ambapo baada ya
kutimiza azima yao walikimbilia kusikojulikana
Afisa
mtendaji wa kijiji cha Rulenge Bw Edson Metusela Gachocha amemtaja
mfanyabiashara aliyevamiwa kuwa ni Ibrahimu Abdalah Bijampora , nakuongeza kuwa
majambazi hayo yalivamia nyumba ya Bw.
Bijampora yakiwa na Silaha za moto na jadi ambapo yalivamia sebuleni wakati yeye na familia yake wakifuatilia
Taarifa ya habari kwenye Luninga
“Mara baada
ya kuingia walianza kushambuliana naye ambapo aliwataka wamuachie awatafutie
fedha na walipokubali aliingia ndani na kufanikiwa kuwatoroka , ndipo walimkaba
mke wake na kuondoka na fedha hizo”alisema
Hata hivyo
mmoja wa wafanya biashara wa mji mdogo wa Rulenge Ruguge Nzutu Ruguge amewataka
wajasiriamali kuimarisha ulinzi wa maeneo ya shughuli zao ili kuhakikisha
usalama unapatikana katika sikukuu za chrismas na mwaka mpya
Katika miaka
ya hivi karibuni imekuwa kawaida ya kipindi chwa mwishoni mwa mwaka kuelekea
siku za Krismas na mwaka mpya matukio ya uharifu hasa uporaji wa fedha kwa
wafanya biashara kutokea, hali inayolitaka jeshi la Polisi pia kuimarisha
usalama
Katika hatua
nyingine Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Revina Alex (36) mkazi wa
kijiji cha Rulenge wilayani humo amelazwa katika Hospitali ya Misheni Rulenge
baada ya kujeruhiwa na majambazi kwa
kumkata mapanga kichwani
Diwani wa
kata ya Rulenge Bw Hamis Baliyanga amesema kuwa mwanamke huyo alijeruhiwa na
watu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliovamia nyumbani kwake na kupora mali ambayo thamani yake
haijajulikana
Baliyanga amesema
kuwa majambazi hayo yalimvamia saa nane usiku kupitia mlango wa nyuma ya nyumba
ambapo walifungua mlango kwa kutumia nondo na kuingia ndani
Jeshi la
polisi wilayani Ngara limethibitisha kutokea kwa matukio yote mawili na kwamba linaendelea na msako mkali
kuwabaini wahusika pamoja na kutoa wito kwa wananchi kujenga tabia ya kutoa
ushirikiano kwa jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za viashiria vya
uharifu
No comments:
Post a Comment