August 14, 2012

Habari Kutoka Radio Kwizera

Burudika,Elimika na RKL FM tembelea www.radiokwizera.com na isikilize kupitia www.radiostationstz.com
Watendaji wa serikali kakonko wasaidie wakulima
KAKONKO
Mkuu wa wilaya ya kakonko mkoani kigoma bw Peter Kiroya,amewaagiza maafisa watendaji wa kata na madiwani wilayani humo kuwasaidia wakulima waliopewa mikopo ya materekita kwa leongo la kuinua  kilimo hapa nchini.
Bw Kiroya ametoa agizo hilo wakati akiongea na viongozi katika kikao cha pamoja kilichofanyika ofisini kwake mjini kakonko.
Amesema serikali wilayani Kakonko kwa kushirikiana na wizara ya kilimo imelenga, kuwainua wakulima na njia nzuri ni kumuondoa katika jembe la mkono, ambalo haliwezi kumsaidia
Bwana kiroya amesema tayari ofisi yake imewasiliana na Suma jkt na kueleza kuwa wako tayari  kumkopesha mkulima atakayeweza kulipia
Watendaji wa serikali wasaidie wakulima
KAKONKO
Mkuu wa wilaya ya kakonko mkoani kigoma bw Peter Kiroya,amewaagiza maafisa watendaji wa kata na madiwani wilayani humo kuwasaidia wakulima waliopewa mikopo ya materekita kwa leongo la kuinua  kilimo hapa nchini.
Bw Kiroya ametoa agizo hilo wakati akiongea na viongozi katika kikao cha pamoja kilichofanyika ofisini kwake mjini kakonko.
Amesema serikali wilayani Kakonko kwa kushirikiana na wizara ya kilimo imelenga, kuwainua wakulima na njia nzuri ni kumuondoa katika jembe la mkono, ambalo haliwezi kumsaidia
Bwana kiroya amesema tayari ofisi yake imewasiliana na Suma jkt na kueleza kuwa wako tayari  kumkopesha mkulima atakayeweza kulipia asimia 30 ya gharama ya trekta.
Aidha amesemakuwa mchakatohuo ufanyike haraka,ili trekta hizo zizinduliwe october 6 wakati wa sherehe za uzinduzi wa wilaya hiyo.   EndS
Wakazi wa mipakani walia na muingiliano wa simu za nje
NGARA
Ukosefu wa mawasiliano ya uhakika katika tarafa ya Murusagamba wilaya ya Ngara mkoani Kagera ni moja ya changamoto inayowakabiliwa wakazi wa tarafa hiyo ikiwa ni pamoja na huduma za kibenki
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakazi wa tarafa hiyo wakati wakizungumza na redio kwizera kwa nyakati tofauti wakidai mitandao ya simu ya Tanzania inaingiliwa na mitandao simu kutoka nchi jirani ya Burundi
Bw Erick Lomward makazi wa tarafa hiyo amesema mtandao wa Vodacom huingiliwa na mitandao ya nchi jirani hali inayosababisha wananchi kushindwa kuwasiliana na wenzao na kupata huduma mbalimbali
Diwani wa viti maalumu wa tarafa hiyo Bi Rehema Ramadhani amependekeza mitandao ya Voda na Airtel kupanua mawimbi yake ya mawasiliano hasa maeneo ya mipakani ili kudhibiti mitandao ya nchi jirani isiathiri wakazi wa tarafa hiyo
Waislamu wilayani kasulu watakiwa kushiriki sensa
KASULU
Waumini wa dini ya kiisilam wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kushiriki katika zoezi la sensa linalotarajia kuanza agositi 26 mwaka huu
Kauli hiyo imetolewa na Shekh Maoud Kikoba wa wilaya ya Kasulu wakati akizungumza na Radio Kwizera wilayani kasulu
Shekh Kikoba amesema waisilamu wanapaswa kutambua kuwa kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi siyo dhambi hivyo wanao wajibu wa kushiriki katika zoezi hilo muhimu
Aidha Shekh Kikoba amewataka wafuasi wa dini ya kiisilamu wilayani kasulu kuachana na uvumi unaowataka kususia zoezi hilo na badala yake washiriki katika sensa hiyo ya watu na makazi kwa kuwa inawalenga watanzania wote
Mbunge wa Mtama aula Bunge la Afrika
DODOMA
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemchagua Mbunge wa Mchinga mkoani Lindi Bw Said mtanda kuwa miongoni mwa wawakilishi wa Tanzania katika bunge la Afrika
Bw Mtanda ambaye amechaguliwa kwa kura 145 dhidi ya 75 alizopata Mbunge wa jimbo la Nzega Dr Hamis Kingwangalla amesema atakuwa mwakilishi mzuri wa Tanznaia katika bunge la afrika
Bw Mtanda amechaguliwa kuchukua nafasi ya Mbunge wa Shinyanga mjini Bw Steven masele ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa naibu waziri wa nishati na madini.                                     EndS
Zaidi ya asilimia 80 wa wanaume wenye ndoa wana nyumba ndogo
NGARA
Utafiti wa shirika lisilokuwa la kiserikali  linalojihusha na utoaji wa elimu  kwa  familia, Global  Family  Enlightment  Organization  umebaini kuwa zaidi ya  asilimia  88 ya wanaume walio katika ndoa  mkoani Kagera wana wake wengine  pembeni maarufu kama nyumba  ndogo.
Mkurugenzi  wa shirika hilo  mkoani kagera  Bw  Inocent  Bideberi  ameiambia radio kwizera mjini Ngara kuwa  hali hiyo inarejesha nyuma maendeleo ya familia kwani wahusika wanashindwa kuhudumia familia zao
Bw  Bideberi  amesema  utafiti umeonyesha kuwa   wanaume wangi  wamekuwa na mwanamke zaidi ya mmoja.
Amesema shirika lake limeandaa  mpango wa kuanza kutoa elimu  kwa jamii   ili kufahamu madhara ya kuwa na nyumba ndogo kwa familia.                            EndS

Serikali yasisitiza uamuzi wake juu ya ushuru wa wachuuzi
KIGOMA
Serikali imesisitiza kuwa hakuna halmashauri inayoruhusiwa kuwatoza ushuru wachuuzi wadogo kwa kuwa imeanzisha ruzuku maalum itakayofidia pengo linalotokana na kufuta kwa kodi kero kwa wananchi
Naibu waziri wa Tamisemi Bw Agrey Mwanri amesema hayo alipofanya ziara maalum mkoani Kigoma kufuatia halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji kugoma kutekeleza agizo lake la kuitaka kuacha kukusanya ushuru kwa wachuuzi wadogo alilolitoa Julai 22 mwaka huu.

Akiongea jana kwenye kikao na uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji, Bw Mwanri amesisitiza kauli ya serikali kwamba hakuna kutoza ushuru kwa wachuuzi wadogo
Aidha naibu waziri Mwanri amewataka baadhi ya wafanyabiashara kuacha kuwapotosha wengine kuwa waziri amesema kwamba wasilipe ushuru. EndS
Wilaya ya Kasulu ina utajiri wa madini ya Nickel
DODOMA
Serikali imesema wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma iko katika uwanda ambako madini aina ya Nickel, Shaba na Chuma
Naibu waziri wa nishati na madini Bw Teven masele amesema hayo bungeni mjini Dodoma leo wakati akijibu swala la mbunge wa Kasulu Mjini Bw Moses Machali
Hata hivyo Bw Masele amesema wilaya ya Kasulu ina madini mengine aina ya Opol, Agate na madini ya ujenzi ya kama vile, mawe, mchanga na changarawe
Katika swali lake Bw Machali alitaka kufahamu tafiti za madini zinaonyesha kuwepo kwa aina zipi za madini katika wilaya ya kasulu iliyoko mkoani Kigoma.
EndS

Jitihada za kutafuta helkopata za Jeshi la Uganda, zaanza
KAMPALA
Helkopta tatu za Jeshi la Uganda zimepotea tangu jana wakati zikiwa njiani kuelekea Somalia kushiriki katika operation ya kijehsi katika mji wa Kismayu
Habari zinasema kuwa helkopta hizo aina ya MI 23 zimepitea wakati nyingine ya nne imenguka wakati akitua nchini Somalia
Gazeti la daily Monitrtor la Uganda toleo la leo limesema helkopta hizo zimepotea kutoka kwenye rada wakati zikiwa kwenye anga la Kenya
Jeshi la Uganda limekaririwa na shirika la habari la Uingereza Reuters likieleza kuwa jitrihada za kutafuta helkopata hizo zinaendelea.               EndS


Wakazi wa mipakani walia na muingiliano wa simu za nje
NGARA
Ukosefu wa mawasiliano ya uhakika katika tarafa ya Murusagamba wilaya ya Ngara mkoani Kagera ni moja ya changamoto inayowakabiliwa wakazi wa tarafa hiyo ikiwa ni pamoja na huduma za kibenki
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakazi wa tarafa hiyo wakati wakizungumza na redio kwizera kwa nyakati tofauti wakidai mitandao ya simu ya Tanzania inaingiliwa na mitandao simu kutoka nchi jirani ya Burundi
Bw Erick Lomward makazi wa tarafa hiyo amesema mtandao wa Vodacom huingiliwa na mitandao ya nchi jirani hali inayosababisha wananchi kushindwa kuwasiliana na wenzao na kupata huduma mbalimbali
Diwani wa viti maalumu wa tarafa hiyo Bi Rehema Ramadhani amependekeza mitandao ya Voda na Airtel kupanua mawimbi yake ya mawasiliano hasa maeneo ya mipakani ili kudhibiti mitandao ya nchi jirani isiathiri wakazi wa tarafa hiyo
Waislamu wilayani kasulu watakiwa kushiriki sensa
KASULU
Waumini wa dini ya kiisilam wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kushiriki katika zoezi la sensa linalotarajia kuanza agositi 26 mwaka huu
Kauli hiyo imetolewa na Shekh Maoud Kikoba wa wilaya ya Kasulu wakati akizungumza na Radio Kwizera wilayani kasulu
Shekh Kikoba amesema waisilamu wanapaswa kutambua kuwa kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi siyo dhambi hivyo wanao wajibu wa kushiriki katika zoezi hilo muhimu
Aidha Shekh Kikoba amewataka wafuasi wa dini ya kiisilamu wilayani kasulu kuachana na uvumi unaowataka kususia zoezi hilo na badala yake washiriki katika sensa hiyo ya watu na makazi kwa kuwa inawalenga watanzania wote
Habari za zamani
 
Kamati ya kuchunguza Rushwa ya wabunge kufanya kazi siku 14
DODOMA
Spika wa Bunge Bi Anna makinda ameunda kamati ya wabunge watano kuchunguza tuhuma kuwa baadhi ya wabunge wanajihusisha na vitendo vya rushwa na kulihujuu sharika la ugavi wa umeme nchini TANESCO
Akiongea bungeni mjini Dodoma Leo Bi Makinda amesema tume hiyo itaongozwa na mbunge wa Jimbola Mlalo Brigedia Jenerali mstaafu Hassan Ngwilizi
Amesema kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa siku 14 kwa kuwaita watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mnadhimu wa upinzani Bungeni bw Tundu Lissu ambaye aliwataja wawabunge sita wenye maslahi katika TANESCO
Sakata hilo lilianza mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara ya nishati na madini ambapo ilidaiwa kuwa baadhi ya wabunge wanapokea rushwa ili kuishawishi Serikai itoe zabuni kwa kampuni zinaotoa fedha hizo. EndS

Kata 16 kibondo na kakonko kutoa maoni ya katiba
KIBONDO
Tume ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuundwa kwa katiba mpya itakusanya maoni katika Kata 16 kati ya 28 zilizoko katika wilaya za kibondo na kakonko mkoani Kigoma
Katibu tawala wa wilaya ya kibondo bw Julius Samwel ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya sherehe kwa ajili ya maandalizi ya ujio wa mwenge wa uhuru kilichofanyika katika ukumbi wa vijana ulioko kibondo mjini
Aidha bw samwel amewataka viongozi wa madhehebu na vyama vya siasa kuendelea kusisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi ili waweze kutoa maoni  yao juu ya kuundwa kwa katiba mpya.              MWISHO

Wana CCM watano wachukua fomu za kugombea uongozi- Ngara
NGARA
Jumla ya Wanachama  watano  wa chama cha mapinduzi  CCM  Wilayani Ngara  wamechukua  fomu za  kugombea  nafasi za uongozi ndani ya chama hicho
Katibu wa  chama cha mapinduzi   Wilayani Ngara  Bi H aulla Kachwamba amesema   zoezi la  kuchukua fomu limeanza jana  na litamalizika   August 6  katika   ya nafasi ya uwakilishi  ndani ya chama
Bi  Kachwamba  ametaja  nafasi  zinazogombewa kuwa ni pamoja na, katibu siasa na uenezi wa wilaya, katibu wa uchumi na fedha ,wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa,wajumbe wa mkutano mkuu  wa taifa na halmashauri ya  wilaya
Aidha   Bi Kachwamba  amesema  nafasi  ya mwenyekiti  wa  CCM ngazi ya wilaya na mjumbe wa  mkutano mkuu wa taifa, fomu  zitaanza kuchukuliwa  kuanzia  August   22   na  28 mwaka huu.              EndS
Uchomaji moto misitu waandaliwa filamu
KIGOMA
Tanzania ni mojawapo kati ya nchi ambazo zinachukuliwa filamu maalum itakayotumika kutoa elimu na mbinu za kuzuia moto misituni kama kampeni ya kuzuia moto duniani.
Kwa kutambua madhara yanayotokana na uchomaji moto ovyo, wizara ya maliasili na utalii kwa kushirikiana na shirika la chakula na kilimo duniani FAO na ubalozi wa Finland  wameandaa mkakati wa mawasiliano wa kuzuia moto nchi nzima
Kijiji cha Kazuramimba kilichopo wilaya mpya ya Uvinza mkoani Kigoma kimepata nafasi ya kuchaguliwa kuwa eneo la kufanyia majaribio ya mkakati huo kwa nchi nzima
Akiongea katika uzinduzi wa makakati huo mkuu wa wilaya ya Uvinza bi.Hadija Nyembo amewataka wakazi wa kijiji hicho kuchukua hatua kuzuia moto
Aidha bi.Nyembo amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika mkakati huo ikiwa ni pamoja na kuwafichua wanaochoma moto ovyo.  EndS
Mahakamani kwa kumuoa mwanafunzi wa kidato cha kwanza
NGARA
Mtu mmoja amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Ngara kwa kosa la kumkatisha masomo mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Mursagamba iliyoko wilayani humo
Mbele ya mlinzi wa amani Bw Zakaria Nyahende, mwendesha mashtaka wa polisi Tumaini Membi, amemtaja mshtakiwa kuwa ni  Chales Shija mwenye umri wa miaka 40 mkazi wakijiji cha Murubanga kata ya Bukirilo wilayani Ngara.
Amesema Januari 23 mwaka huu katika eneo la Murubanga, mshitakiwa  alimkatisha masomo mwanafunzi wa kidato cha kwanza na kuishi naye kama mke wake
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwani alikuwa mbele ya mlinzi wa amani ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agoust 16 mwaka huu.   EndS

Wakazi wa Kigoma watakiwa kujihadhari na Ebola
KIGOMA
Mkuu wa mkoa wa Kigoma luteni kanali mstaafu Issa Machibya amewataka wakazi wa mkoa huo kuchukua tahadhari ya kuepuka ugonjwa wa Ebola kwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa mitano ya Tanzania iliyoko jirani na nchi ya Uganda ambako kuna mlipuko wa ugonjwa huo
Tangu kulipuka tena kwa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa chini ya Uganda takriban watu 20 wamepata maambukizo na 16 wamepoteza maisha. EndS
Kizimbani kwa kuendesha gari na kusababisha kifo
NGARA
Raia wa Rwanda amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa kosa la kuendesha gari kwa njia ya hatari na kusababisha kifo
mshtakiwa Andrew Rudasingwa mwenye umri wa miaka 40 na mkazi wa Kigali anashitakiwa kwa kusababisha kifo cha mwanaidi Ismail
Mbele ya mlinzi wa amani Bw Zakaria Nyahende mwendesha mashtaka wa polisi Tumaini Membi amesema tukio hilo limetokea Julai 31 mwaka huu majira ya saa 7:40 katika eneo la Rusumo wilayani Ngara.
Amesema mshtakiwa aliendesha  Lori aina ya Mercedes benzi bila uangalifu na kugonga kibanda alichokuwemo Bi mwanaid Ismail hali iliyopelekea kifo cha mtu huyo
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwani alikuwa mbele ya mlinzi wa amani ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agoust 16 mwaka huu ambapo mshtakiwa amepelekwa rumande.                     EndS


Kigoma yajipanga kufanikisha Sensa
KIGOMA
Mkoa wa Kigoma umejipanga kuhakikisha kuwa zoezi la sensa ya watu na makazi linafanikiwa mkoani humo.
Mwenyekiti wa Sensa mkoani Kigoma ambaye pia ni mkuu wa mkoa huo luteni kanali mstaafu Issa Machibya amesema watahakikisha kila mtu mkoani humo anahesabiwa wakati wa zoezi hilo litakalo anza Augosit 26 mwaka huu
Aidha luten kanali Issa Machibya ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa makarani na wasimamizi wa sensa ili waweze kuhesabiwa
Pia amewataka wale wote ambao kwa sababu moja au nyingine hawatakuwepo katika kaya zao siku ya sensa kuacha kumbu kumbu zao ili makarani wa sensa waweze kuzifanyia kazi.                                      EndS

Mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi wafukuta
DAR ES SALAAM
Serikali ya Tanznaia imependekeza kupatikana kwa suluhisho la mgogoro baina ya yake na Malawi juu ya uamuzi wa kutafuta mafuta na gesi katika ziwa Nyasa
Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa  bw Benard membe amesema serikali ya Tanznaia itaendelea kufanya mazungumzo na Malawi inayodai kuwa Ziwa Nyasa ni mali yake
wiki uiliyopita bw Membe alisema kuwa shughuli za kutafuta mafuta na gesi katika Ziwa Nyasa ambazo zinaendeshwa na Malawi hazina budi kusitishwa ili kutafuta suluhu la mgogoro wa umiliki wa ziwa hilo
serikali ya Malawi inatumia mkataba wa mwaka 1890 ambao unaeleza kuwa mpaka wa Tanznaia unaishia kwenye fukwe ya ziwa Nyasa ndani ya eneo la Tanzania.                                   EndS



Kimataifa
Tume ya uchaguzi Kenya kuepuka udanganyifu katika uchaguzi  
NAIROBI
Tume ya uchaguzi ya Kenya imesema kuwa itachukua hatua ili kuepuka vitendo vya udanganyifu wakati wa uchaguzi mkuu ujao nchini humo
Tume hiyo imepanga kununua vifaa vyenye thamani ya shilingi bilioni 3.9 kwa ajili ya kutambua alama za vidole pamoja na sura za wapiga kura
Imesema kuwa vifaa hivyo vitaondoa udanganyifu kama uliofayika kwenye uchaguizi mkuu uliopita na matokeo yake yalipelekea machafuko
Aidha tume hiyo imepenga kuandikisha wapiga kura milioni 18 kwa ajili ya uchaguzi huo ambaoutafanyyia mwezi march mwaka kesho.              EndS

Jeshi la Syria laharibu mawasiliano ya waasi
DAMASCUS
Jeshi la Syria limefanikiwa kuharibu mtambo wa mawasiliano ya simu wa waasi uliotolewa na serikali ya Uturuki
Mtambo huo umeharibiwa huku mapigano yakiendelea katika mji wa Allepo kati ya majeshi ya serikali na waasi
Aidha Jeshi la Syria linaendelea kufanya doria katika mji wa Damascus pamoja na Homs ili kuwasaka waasi
Habari zinasema kuwa zaidi ya waasi 50 wameuawa katika mji wa Damascus huku wengine kadhaa wakikamatwa.                      EndS
Wapiganaji wanne wauawa Afghanistan  
KABUL
Vikosi vya Usalama vya Afghanistan vimewaua wapiganaji wanane wanaosadikiwa kupanga njama za mashambulizi katikati ya mji wa Kabul
Maofisa wa usalama walivamia nyumba moja iliyoko masharki mwa mji huo ambapo walifanya mapambano ya risasi na kufanikiw akuwaua watu wanane
Maofisa wamefanikiwa kukamata magari yanayosadikiwa kuwa na milipuko katika tukio hilo ambalo limetokea leo
Mkuu wa Jeshi la Polisi katika mji wa Kabul jenerali Mohamed Ayub Salangi amesema wapiganaji wengine watatu wamekamatwa jana usiku wakiwa na milipuko.                EndS

ICTR yakabidhi nyaraka kwa Rwanda
KIGALI
Mahakama ya kimataifa ya mauaji ya halaiki ya Rwnada ICTR imekabidhi nyaraka za kesi za mauaji ya halaiki zinazowakabili Alloys Ndimbati na Charles Ryandekayo.
Mamlaka ya waendesha mashitaka ya Rwanda imesema ICTR yenye makao yake nchini Tanzania imechukua hatua hiyo wakati mahakama hiyo ikikamilisha majukumu yake  baada ya mkufanya kazi kwa miaka 18
Mkuu wa kitengo cha rufaa cha mahaka aya ICTR Bw James Arguin amekabidhi nyaraka hizo kwa mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali ya Rwnada Bw Martin Ngoga
watuhumiwa ambao hata hivyo hawajapatikana wanadaiwa kuhusika na mauaji yaliyotokea kwneye mji wa Kibuye nchni Rwnada mwaka 1994.                             EndS

Ugonjwa wa Ebola waendelea kuitesa  Uganda
KAMPALA
Wizara ya afya ya Uganda imesema watu wengine wawili wamefariki juzi  jioni kutokana na ugonjwa wa Ebola
Taarifa ya wizara ya afya imesema vifo hivyo vimetokea katika hospitali ya Kagadi iliyoko wilaya ya Kibaale
Taarifa hiyo imesema idadi ya waliofariki imefikia 16 tangu mwezi july mwaka jana ambapo ugonjwa ebola ulitokea nchini Uganda
Imesema kuwa wagonjwa wawili waliolazwa kwneye hospitali ya kagadi wamethibitia kuwa na ugonjwa wa Ebola.             EndS
Habari July 31,2012
Mgomo wa walimu waingia siku ya pili
NGARA
Mgomo wa walimu umeingia siku ya pili  ambapo wanafunzi wameendelea kuwa wahanga wa mgomo huo
Katika manispaa ya kigoma ujiji chama walimu  CWT mkoani Kigoma kimesema walimu wote wameitikia wito wa kugoma.
Licha ya taarifa za kuwepo kwa baadhi ya walimu kutoitikia mgomo huo katibu wa CWT mkoani Kigoma bw.Emmanuel Samala amesema walimu wote wameunga mkono mgomo huo.
Hata hivyo baadhi ya walimu katika manispaa ya Kigoma Ujiji wameendelea kutekeleza majukumu yao kama kawaida kwa kile walichoeleza kuwa wao sio wanachama wa CWT hivyo hawawezi kushiriki katika mgomo huo.
Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Buteko Fortunatus Mpaze amesema hakuna mwalimu aliyegoma na kwamba walimu wote wamefika shuleni na wanaendelea na majukumu yao.
wilayani Ngara,   baadhi ya  wanafunzi  katika  shule  za msingi na sekondari wameonekana wakicheza  kutokahna na kukosa walimu wa kuwafundisha
Radio  kwizera  imetembelea shule za msingi Ngara mjini, Nyamiaga ,Mumiterama  na  kushuhudia  wanafunzi  wakicheza    huku  baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba wakiwafundisha wenzao
Baadhi  ya wanafunzi wa  darasa la  saba  katika  shule ya msingi Ngara mjini  wameilaumu serikali kwa kushindwa kutatua  madai ya walimu na kueleza kuw aheunda wakashindw akufanya vizuri katika mitihani ya taifa
Mwalimu  mkuu wa shule  ya msingi  Ngara mjini  Bw  Charles Fukumbe  ambaye  alikuwa  mwalimu pekee shule hapo amesema  walimu  wote wanatekeleza mgomo huo
Wilayani kasulu,  Wazazi wilayani kasulu mkoani kigoma wameiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa mgomo wa walimu kwani watoto wao ndio waathirika
Wakiongea na radio kwizera, wazazi hao wameiomba serikali kuzungumza na walimu ili kutafuta ufumbuzi wa haraka kwani mgomo huo unawanyima watoto wao haki ya msingi ya kupata elimu
Mmoja wa wazazi hao Bw: Wilagaza Makulazo, amesema mgomo huo unaathiri maendeleo ya watoto wa hasa kwa wanaotarajiwa kufanya mitihani ya taifa
Aidha wazazi hao wameiomba serikali kufanya jitihada za haraka kutafuta ufumbuzi wa mgomo huo kwani utaathiri misha ya watoto wao
Na, katika wilaya ya Biharamulo mkoani kagera, Uongozi wa kijiji cha Ngararambe umetoa wito kwa serikali kutoa tamko la kuwataka wanafunzi wasiende shuleni katika wakati huu ambapo mgomo wa walimu unaendelea
Mwenyekiti wa kijiji cha Ngararambe Bw Yusuph Seif amesema maisha ya wanafunzi yanaweza kuw ahatarini katika shule zilizoko kwneye barabara kuu kwani wamekuwa wakicheza bila uangalizi
Bw Seif amesema walimu katika shule ya msingi Mzani yenye wanafunzi 1400 wamegoma kufika shuleni na kubali mwalimu mkuu pekee ambapo wanafuzi wamekuwa wakicheza karibu na barabara kuu ya Isaka- Kigali na Bujumbura hivyo uhatarisha maisha yao
Bw Seif amesema serikali haina budi kuwazuia wanafunzi kufika shuleni au kutafuta haraka ufumbuzi wa mgomo wa walimu ambao umeanza jana nchi nzima.                                                  EndS

Mkazi wa Kibondo auawa kwa kupigwa risasi
KIBONDO
Watu wanao sadikiwa kuwa ni majambazi wamemuua kwa kumpiga rissi Mkazi wa Kijiji cha Samvula Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma
Taarifa ya polisi imemtaja aliyeuawa kuwa ni Bw. Buchumi Julias mwenye umri wa miaka 46 ambapo imeelezwa kuwa watu hao walimpiga risasi akiwa nyumbani kwake
Tukio hilo limetokea usiku wa July 29 mwaka huu ambapo imelezwa kuwa watu hao hawakuchukua chochote baada ya kufanya mauajihayo
Aidha mpaka sasa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na kwamba jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kuwabaini waliofanya mauaji hayo. EndS

Kizimbani kwa kumpa ujauzito mwanafunzi
NGARA
Mtu mmoja amefikishwa katika mahakama ya wilaya Ngara kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi wa wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Ntobeye iliyoko wilayani Ngara mkoani kagera
Mbele ya mlinzi wa amani Bw Zakaria Nyahende mwendesha mashtaka wa polisi Tumaini Membi amemtaja mshtakiwa kuwa ni Jafeth Isaya mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa kijiji cha Murunyinya wilayani humo.
Amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo March 19 mwaka huu katika kijiji cha Ntobeye wilayani Ngara
Hata hivyo mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwani alikuwa mbele ya mlinzi wa amani ambapo,kesi hiyo imeahirishwa hadi Agoust 14 mwaka huu itakatapotajwa tena.               EndS

 10 mbaroni kwa ujambazi wa kutumia silaha- Geita
GEITA
Jeshi la polisi mkoani Geita limewakamata watu 10 wakituhumiwa kwa uhalifu wa kutumia silaha katika matukio yaliyotokea hivi karibuni kwenye wilaya za Nyang’hwale, Chato na Mbongwe mkoani humo.

Kamanda wa polisi mkoani Geita Leonard Paul amesema katika sako huo mtu mmoja Katika kijiji cha Igalula kata ya Kasenga wilayani Chato katika   mapambano na polisi ambapo bunduki mbili ziikamatwa

Aidha katika kijiji cha Nyamikonze wilayani Nyang’hwale watuhumiwa watatu walikamatwa kwa kujihusisha na mauaji yaliyotokea hivi karibuni

Katika msako huo pia, watu sita, wamekamatwa baada ya kuvunja na kuiba katika kijiji cha Bugalagala kata ya Ikobe wilayani Mbongwe

EndS
 Lissu hawezi kushitakiwa- Makinda 
DODOMA
Spika wa bunge Bi Anna Makinda amesema mbunge wa Singida mashariki bw Tundu Lissu ana kinga ya kutoshitakiwa kufuatia kuwataja wabunge wanaotuhumiwa kunufaika kupitia shirika la Umeme nchini TANESCO
Bi makinda amesema hayo bungeni mjini Dodoma kujibu mwongozo wa mbunge wa Simanjro Bw Christopher Ole Sendeka ambaye alitaka mwongozo ili aweze kufungua kesi mahakamani
Amesema eneo ambalo mbunge huyo alitumia kuwataja wabunge saba kwa tuhuma za rushwa lina kinga ya kibunge hivyo hawezi kushitakiwa
Hapo Jana Bw Lissu aliwataja wabunge, Christopher ole Sendeka, Charles Mwijage, Vicky kamata, Sarah Msafiri, Munde Tambwe, Yusuf Abdallah Nasri   na Mariam Kisanji kuwa wanajinufaisha kupitia TANESCO
EndS
Kimataifa
Ebola yaendelea kutesa Uganda
KAMPALA
Watu wengine sita wamaosadikiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola wamelazwa hospitali ikiw ani siku chache baada ya kubainika kuwepo kw amlipuko w augonjwa huo katika eneo la magharibi mwa Uganda
Afisa wa afya katika wilaya yak abele nchini Uganda bw Stephen Byaruhanga amesema ugonjwa wa Ebola ambao awali ulikuwa katrika kijiji kimoja hivi sasa umesambaa katika vijiji vingine vya wilaya hiyo
Akilihutubia taifa hapo jana Rais, Yoweri Museveni ametoa tahadhari kw awananchi kuepuka kugusana bila sababu ya muhimu na kutoa taarifa mapema ikiwa watambaini mtu mwenye dalili za ugonjwa huo
Maofisa wa wizara ya afya ya Uganda pamoja na shirika la afya la umoja wa mataifa WHO wamesema kuwa watu 14 wamekufa nchini humo kutokana na Ugonjwa wa Ebola.                                EndS


Katibu mkuu wa wizara kizimbani kwa Rushwa
KIGALI
Katibu mkuu wa wizara ya serikali za mitaa katika serikali ya Rwanda Bw Cyrille Turatsinze, amefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya rushwa yanayomkabili
Turatsinze alikamatwa July 21, akidaiwa kuomba rushwa ya faranga milioni mbili kutoka kwa mfanyabiashara ili amwezeshe kupata zabuni ya kusambaza vifaa vya kompyuta katika wizara ya serikali za mitaa
Katibu mkuu huyo amefikishw akatiaka mahakama ya mjini Kigali pamoja na mshirika wake Rwego Harelimana, ambaye alipokea malipo ya awali ya faranga laki tano
Mbele ya Jaji Maliciane Mukagasana, washitakiwa wamesema kuwa wanahitaji muda wa kupitia mashitaka yao kabla ya kujibu chochote
kufuatia hali hiyo Jaji Mukagasana aliahirisha kesi hiyo hadi keshokutwa ambapo washitakiwa wamerejeshwa rumande.                           EndS

Serikali ya DRC yatakiwa kupitia upya mkataba wake na waasi
KINSHASA
Gavana wa jimbo la Kivu kaskazini lililoko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC ameitaka serikali ya nchi hiyo kufanya tathimini ya makubaliano ya March mwaka 2009 ambayo yamepelekea uasi katika jimbo hilo
Makubaliano ya March 23 mwaka 2009 yalipelekea waasi kujiunga katika jeshi la Serikali lakini mwezi April mwaka huu mamia ya waasi hao walijiondoa kwenye jeshi na kuunda kundi linalo fahamika kama M23
Gavana huyo Julien Paluku Kahongwa amesema kupitiwa kwa mkataba huo kutatoa fursa kwa Rais Joseph kabila kutekeleza ahadi yake ya kupatia ufumbuzi wa kisiasa mgogoro huo
Waasi hao wamekuwa wakiendesha mapigano dhid ya jeshi la Serikali ya DRC huku ikidaiwa kuwa wanapata msaada kutoka kwa serikali ya Rwanda.                                 EndS

Clinton aanza ziara barani Afrika
WASHINGTON
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Bi Hillary Clinton anatarajiwa kuzuru Sudan ya Kusini ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 11 katika bara la afrika ambayo inanatarajiwa kuanza wiki hii
Katika ziara hiyo ambayo inaanza leo kwa kutembelea Senegal, Bi Clinton anatarajiwa kuhamasisha ukuaji wa uchumi pamoja na  kuimarisha amani na usalama
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi z anje wa Marekani Bi Viktoria Nuland amezitaja nchi nyingine ambazo waizri huyo atazitembelea kuwa ni Uganda, Kenya, Malawi, na Afrika kusini
Akiwa nchini Senegal, Bi Clinton atakutana na rais Macky Sall ambaye muungano wa vyama vya siasa unaomwunga mkono umeshinda katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika hivi karibuni      EndS
Majeshi ya Syria yapambana na waasi
DAMASCUS
Majeshi ya Syria yanaendelea kuwashambulia waasi ambao wamejificha katika mji wa Allepo ulioko nchini humo
Habari zinasema kuwa hospitali za mji huo zina idadi kubwa ya majeruhi wanaotokana na mapigano ahyao ambayo yameingia siku ya nne
Maelfu ya watu wanaendelea kuukimbia mji huo hali ambayo imepelekea kuwepo kwa janga la kibinadamu
Wakati huo huo Marekani na Uturuki zimekubaliana kuongeza jitihada ili kufikiwa kwa mabadiliko ya kisiasa nchini Syria
Ikulu ya Marekani imesema kuwa mabadiliko hayoyatahusisha kuondoka madarakani kwa Rais Bashar al-Assad wa Syria.                           EndS

Habari 30,07.2012
Madhehebu ya dini yashauriwa kuondoa tofauti zao
KIBONDO
Askofu mkuu wa kanisa Anglican la kiinjili tanzania EACT Ainea Kusehna ametoa wito kwa madhehebu kuondoa tofauti zao ambazo zinaweza kuchochea migogoro mbali mbali katika jamii
Askofu Kusehna amesema hayo wakati wa ibada ya kuwasimika makanoni wawili pamojana na mashemasi iliyofanyika katika kanisa lililoko eneo la  kitahana wilayani kibondo
Amesema hakuna sheria inayomlazimisha mtu kufuata dini asiyoipenda na badala yake kila mtu anao uhuru wa kuabudu dini anayoipenda
Aidha askofu kusehna amewataka viongozi wa dini kupinga ushoga na ndoa za jinsia moja kwa kuwa ni kinyume na mipangoa ya mwenyezi mungu
Katika ibada hiyo Askofu Kusehna amewasimika wachungaji Joseph Kimoli pamoja na Naftari Mahungiro kuwa makasisi katika kanisa la EACT kata ya kitahana wilayani kibondo. EndS



Mgomo wa walimu wafanikiwa katika maeneo mbalimbali nchini
NGARA
Walimu nchini Leo wananza mgomo kuitikia wito wa chama cha walimu nchini CWT ili kuishinikiza serikali kuboresha maslahi yao
Uchunguzi wa Radio Kwizera katika maeneo mbalimbali nchni umebaini kuwa walimu wengi wameitikia wito wa kugoma kufanya kazi
Uchunguzi katika shule za msingi Ruganzo, Ngara mjini Nakatunga na kumuyange wilayani Ngara umeonesha kuwa walimu wa shule hizo hawakufika shuleni
Aidha katika shule hizo walimu wakuu ndio walioonekana mashuleni huku wanafunzi wafanya michezo mbalimbali
Mwalimu wa shule ya Sekondari Ntobeye  Bw Sharaza Tadeo amesema hawezi kuingia darasani kwa kile alichokieleza kuwa serikali imeshindwa kutatua kero zao
Wilayani Kibondo Chama cha walimu CWT wilayani humo kimewataka wanachama wake kuunga mkono mgomo ambao umeeanza leo
Katibu wa CWT wilayani Kibondo Bw.Lazaro Nkwavu amesema mgomo huo utaendelea hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai yao
Bw. Nkwavu ameyataja baadhi ya madai yao kuwa ni pamoja na nyongez ya mshahara kwa asilimia 100,posho ya kufundishia 55% kwa walimu wa masomo ya Sayansi na asilimia 50 kwa wanaofundisha masomo ya sana
Katibu huyo ameyataja madai mengine kuwa ni Posho ya kujikimu katika mazingira magumu,na kuwataka walimu kutotishika kwa vitisho vinavyotolewa na baadhi ya maafisa wa Serikali
Katika hatua nyingine jumla ya wabunge sita wametaka bunge lisitishe shughuli zake ili lijadili mgomo wa walimuu  ulioanza leo
Wabunge hao wakiongozwa na mbunge Yahya Kassim Issa wamelitaka bunge kusitisha shughuli zake ili lijadili mgomo huo wa walimu wan chi nzima
Naibu Spika wa Bunge  bw Job Ndugai amesema suala hilo haliwezi kujadiliwa kwa kuwa limefikishwa mahakamani
Bw Ndugai amesema taarifa alizopatiwa zinaonyesha kuwa serikali pamja na CWT leo wanawalisha hoja zao katika mahakama kuu ambapo kesho mchana mahakama itaanza kusikiliza madai yao. Ends





Biashara huria yachangia ongezeko la ajali za majini
ZANZIBAR
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema ajali za meli zinazoendelea kutokea zimesababishwa na soko huria la biashara katika sekta ya usafirishaji baharini visiwani humo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed, amesema hayo wakati akifunga mjadala wa taarifa ya serikali kuhusu ajali ya meli ya MV Skagit iliyotokea Julai 18, mwaka huu.
Amesema meli hiyo iliingizwa Zanzibar kutoka Marekani Oktoba, mwaka 2011 ikiwa imebakiza miaka miwili kumaliza muda wa matumizi.
Waziri Aboud, amesema tangu SMZ kuruhusu wafanyabiashara kuwekeza katika sekta hiyo,wapo baadhi ya watu  ambao wamekuwa wakinunua meli chakavu kutokana na kushindwa kumudu gharama za meli mpya.
Amesema serikali imezuia vyombo chakavu vya usafiri kufanya kazi visiwani humo.     EndS


Kamati ya Uongozi ya Bunge yakutana juu ya rushwa kwa wabunge
DODOMA
Kamati ya uongozi ya Bunge imekutana  mjini Dodoma kujadili hatua za kuchukua kutokana na tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi wa wajumbe wa kamati za kudumu za bunge
Naibu Spika wa Bunge Bw Job Ndugai amesemawajumbe wa kamati ya uongozi wa bunge wanakutana na Spika wa Bunge Bi Anna Makinda kujadii tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge
Hatua hiyo imetokana na ombi la mwongozo kutoka kwa wabunge watatu wakiongozwa na Mbunge wa Arumeru mashariki Bw Joshua Nassari  aliyetaka kuvunjwa kwa kamati zote zinazotuhumiwa kwa rushwa
Hatua hiyo imetokana na uamuzi wa mwishoni mwa wiki iliyopita wa Spika waBunge Bi Anna Makinda kutangaza kuivunja kamati ya nishati na madini ya bunge kufuatia taarifa kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya nishati ya madini wanapokea rushwa ili kulihujumu shirika la ugavi wa umeme nchini Tanesco               EndS
Kimataifa
Zaidi ya 1600 wabambwa kwa dawa za kulevya nchini Rwanda
KIGALI
Jumla ya watu 1,663 kati yao 163 wakiwa wanawake wamekamatwa nchini Rwnada katika kipindi cha miezi sita iliyopita kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya
Taarifa ya Polisi imesema zaidi ya watu 1,300 waliokamatwa wana umri wa kati ya miaka 18 na 35
Taarifa hiyo ya Polisi imesema walliokamatw ani pamoja na wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya
Imesema kuwa zaidi ya kilo 1600 za bangi na zaidi ya lita 3,868 za pombe aina ya Kanyanga zimekamatwa katika kipindi hicho
Kabila aituhumu Rwanda kwa kuwasaidia waasi wa DRC
KINSHASA
Rais wa jamhuri ya Kidemokrasi ya kongo DRC bw Joseph kabila ameituhumu Rwnada kwa kuwaunga mkono waasi wa nchi yake
Rwanda inatuhumiwa  kufuatia ripoti ya wataalamu wa umoja wa mataifa kuwa imekuwa ikiwasaidia waasi wa kundi la M23 ambao anakabiliana na wanajehsui wa serikali ya DRC katika jimbo la Kivu ya kaskazini
Akiongea katia kipindi cha television Bw Kabila amesema dunia nzima inafahamu kwmaba Rwnada inawasaidia waasi hao.        EndS
 47 wafariki kwa ajili ya treni nchini India
NEW DELHI
Watu 47 wamefariki  kufuatia ajali ya moto iliyotokea kwenye ya  treni iliyokuwa ikisafiri katika jimbo la Andhra Pradesh nchini India
Behewa moja la treni ya tamilnadu iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa Delhi kwenda Chennai limeshika moto mapema hivi leo ambapo chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika
Maofisa wa serikali wamesema idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka kw akuw abehewa hilo lilikuwa na abiria 72
Ajali hiyo uimetokea wakatri treni hiyo ikiwa kituo cha Nellore kilichoko umbali wa kilomita 500 kusni mwa mji wa Hyderabad
Habari za zamani

July 26,2012
Jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtumishi wa idara ya uhamiaji aliyetoroka akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa wakazi wa kijiji cha Bugarama akidai ni wahamiaji haramu.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Bw Philip Karangi amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtumishi huyo ambaye alitoroka akiwa katika kituo cha polisi cha Bugarama wilayani Ngara.

Mtuhumiwa huyo Edga Cheni Mponi alikuwa afisa uhamiaji katika kata ya Bukirilo kabla ya kumamishiwa katika mkoa wa kigoma mwezi june mwaka huu.

Aidha kamanda wa Polisi mkoani Kagera ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi wilayani Ngara kuhakikisha wanamkamata mtuhumiwa huyo.

Wananchi wilayani Kibondo wametakiwa kuwapa ushirikiano makarani wa Sensa watakaochaguliwa kushiriki katika sensa ya watu na makazi ili kufanikisha malengo ya zoezi hilo.

Mkuu wa wilaya ya Kibondo Bw. Venance Mwamoto amesema hayo katika mkutano na wananchi wa tarafa ya Kifura wilayani Kibondo.

Bw. Mwamoto amesema wananchi wanatakiwa kutambua kuwa sensa ina lengo la kutambua idadi ya wananchi na hali zao ili Serikali iweze kupanga mipango ya maendeleo.

Aidha amewataka viongozi wa Serikali za vijiji na kata kuwahimiza wananchi kujitayarisha kuhesabiwa.


Wakazi watano wa kijiji cha Katoto wilayani Kasulu leo wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kasulu wakikabiliwa na shitaka la kuwatumikisha watoto katika shughuli za kuchunga mifugo kijijini humo.

Mbele ya mlinzi wa amani Rajabu Mtuli mwendesha mashitaka wa polisi Bw. Athuman Mshana amewataja washitakiwa hao kuwa ni Luhamiza Mtasha, Luhwanya Bilala, Kabanya Huhinda, Adamu Huhinda pamoja na Samson Nyanza wote wakazi wa kijiji cha Katoto na kwamba ni wafugaji wa ng’ombe.

Bw. Mshana amesema July 20 mwaka huu watuhumiwa hao walikamatwa na askari wa wanyamapori waliokuwa doria katika hifadhi ya Malagarasi wakiwa na watoto kumi walio na umri kati ya miaka 10 hadi 17 wanaotoka vijiji mbalimbali vya wilaya ya Kibondo.

Washitakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa walikuwa mbele ya  mlinzi wa amani, ambapo kwa sasa wako nje kwa dhamana hadi Agosti 7 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Walimu wa shule za msingi wilayani Chato wametajwa kuwa chanzo cha kushuka kwa taaluma baada ya kushindwa kutengeza mazingira mazuri ya wanafunzi ili waweze kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.

Hayo yamo katika ripoti iliyotolewa na shirika la Uwezo lisilokuwa la kiserikali lililofanya utafiti kuhusu uwezo wa wanafunzi wa kujua kusoma na kuandika ambao ulifanyika katika shule 132 nchini.

Akitoa taarifa hiyo kwenye mdahalo wa kujadili hali ya elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Bw Methew Chungu amesema kuwa wilaya ya Chato imeshika nafasi ya 56 kati ya shule 132.

Bw Chungu amesema kulingana na utafiti huo wanafunzi watatu kati ya 10 wa darasa la tatu hadi la saba hawawezi kusoma sentensi ya kiingereza.


Serikali imeahadi kufanya uhakiki wa vituo vyote vya kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu katika mwaka wa fedha 2012/13 ili kuona hali halisi ya huduma zinazotolewa kwa watoto hao.

Naibu waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dr Seif Rashid amesema hayo leo mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Amesema kuwa mpaka sasa kuna vituo 98 vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu nchini vilivyosajiliwa kwa mujibu wa sheria na kutoa huduma kwa watoto wapatao 3958.

Naibu waziri wa afya alikuwa akijibu swali la mbunge viti maalum Joyce Nkya aliyetaka kufahamu kama serikali inafaya uhakiki wa ubora wa vituo vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu nchini.


Mkuu wa mkoa wa Geita Bw Said Magalula amekutana na baadhi ya wamilika wa magari madogo marufu kama michomoko na kusisitiza kuwa hataruhusu magari hayo kufanya kazi ya kubeba abiria.

Akizungumza jana katika kikao kilichofanyika ofisini kwake mkuu huyo wa mkoa amesema kwamba hawezi kubatilisha agizo hilo kwani tayari limefikishwa ofisi ya waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Hata hivyo mwenyekiti wa chama cha madereva mkoani Geita Bw Emanuel Biramba amewataka madereva kuwa wavumilivu kwani suala hilo linashughulikiwa kwa kufuata taratibu ili kuhakikisha ufumbuzi unapatikana.

Bw Biramba amesema suala hilo wamelifikisha kwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM taifa Bw Nape Nnauye ili waweze kulizungumza katika ngazi ya chama.

Mkuu wa mkoa wa Geita alisitisha magari madogo kufanya kazi ya kubeba abiria maarufu kama mchomoko kufuatia ajali iliyohusisha magari madogo matatu yakiwemo mawili ya abiria na kusababisha vifo vya watu 11 na wengine 12 kujeruhiwa.
…………………………………………………………………………………………………………………… Kusikiliza Redio kwizera LIVE … www.radiostationstz.com …Kisha chagua RK.

No comments:

Post a Comment