July 23, 2012


NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE, TAHADHARI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI TANZANIA 2012.

Na: Juventus Juvenary

Kijana Ngoswe,afisa mhesabu watu toka jijini Dar es salaam,afika kijijini amebeba mikoba miwili.mmoja una nguo zake na mwingine una vifaa vya kuhesabia watu. Anamwona mama mmoja akilima.Anasimama na kuweka chini mikoba yake. Anasimama na kuweka chini mikoba yake na kuanza kujisemea mwenyewe………………kama mtu anasema shamba,basi shamba ndioyi hii,loh!(akitazama huku na huko).vumbi jekundu kama ugoro wa subiana!(ainama na kuanza kuibenjua suruali yake aina ya bell-bottom )…….

Naikumbuka sana hadithi hii ya NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE kutoka katika Kitabu kilichoandikwa na mwandishi Edwin Semzaba na kupelekea mchezo wa radio kupitia kituo cha matangazo Radio Tanzania Dar es salaam enzi hizo RTD kurusha mchezo huo ambao naweza kusema mpaka sasa naona kuna umuhimu mchezo huo kuna haja ya kuurudia kupitia vituo mbali mbali
Ni hadithi iliyowahusisha washiriki wapatao kumi na watano.
NGOSWE:kijana wa kiume,Umri kati ya miaka 25 na 30, MAZOEA:msichana mwenye umri kati ya 18-20,NGENGEMKEMI MITOMINGI:Balozi,MZEE JIMBI:Mwanakijiji,KIFARUHANDE:Mwanakijiji,MAMA MAZOEA:mke wa Mitomingi,MAMAINDA:mke wa Mitomingi,HUZUNI:Mtoto wa Mitomingi,MAMA WA KWANZA:mwanakijiji,MAMA WA PILI:mwanakijiji,CHAPUUKA:mwanakijiji,MTOTO:mwanakijiji,MAMA MASIKIO:mwanakijiji,MZEE WA KWANZA  mwanakijiji na  na MZEE WA PILI:Mwanakijiji
Nimesema naikumbuka sana hadithi na mchezo huu mzuri wenye ujumbe kwa jamii hasa kwa mtindo alioutumia Mtunzi na mwandihi kwa kuigawanya katika mtindo wa Kijito,Vijito,Mto,Jito,na Baharini. Mwandishi Edwini Semzaba alifanya hivyo maksudi kutokana na mtoririko na ukubwa wa Hadithi pia matukio yake

Ni hadithi yenye mafundisho ka Taifa letu Tanzania hasa wakati huu linapoelekea kufanya sensa ya watu na makazi August 26 mwaka huu.
Katika hadithi hii/mchezo wa radio ,Kijana Ngoswe ambaye ni karani wa sensa anasimama katika nafasi ambayo Vijana wa sasa wanaitafuta ili kushiriki katika zoezi la sensa.
Wapo watakao/wamepata nafasi ya kushiriki katika zoezi hilo,wakitegemea kulipwa/kupata malipo ya kazi hiyo kama alivyokuwa ngoswe.

Ngoswe,kwa mujibu wa mwandishi alikuwa kijana nadhifu,hodari na mchapa kazi na kupelekea Taifa kumpa hadhi ya kuwa afisa/kalani wa sensa lakini mwishoni nyaraka zote alizotumia katika zoezi la sensa ziliunguzwa moto hali iliyopelekea taifa kukosa Taarifa na takwimu muhimu zilizotegemewa kutoka eneo alilopangwa kufanya sensa.

Ni tahadhari kuwa inayotakiwa kuchukuliwa na watu mliopata nafasi ya kushiriki katika zoezi la sensa kwa kuepuka matendo ambayo yalimuondolea sifa na heshima aliyokuwa nayo Ngoswe. Kwa wale waliofanikiwa kusoma Kitabu cha NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE mtakumbuka namna Ngoswe alivyojikuta akiingia katika dimbwi la mahaba na Binti wa mzee Mitomingi
Kwa wasomaji wa maandiko matakatifu wanaelezwa kuwa “huwezi kuwatumikia mabwana wawili” Ngoswe hakujali hilo. Alifanya kazi,huku akiwaza mapenzi na Mtoto wa Mitomingi hali iliyopelekea kuamua kutoroka naye huku akizisahau nyaraka muhimu za sensa na baada ya wazazi wa binti kugundua kuwa Binti yao katoroshwa na kalani wa Sensa,wakakasirika na kuziunguza moto

Sensa ni suala n yeti sana katika maendeleo ya taifa. Sensa ndio inayotoa tathimini ya idadi ya watu wa taifa husika,kwahiyo ndio inayoweza kuongoza Bajeti.

Natambua wapo watu mliopata nafasi ya kufanya sensa mwaka huu. Chonde chonde,kule mnakoenda kuhesabu watu kuna mambo mengo. Kuna vishawishi vingi kama alivyokutana navyo NGOSWE. Ngoswe usiku flani alikuwa akitumia Pombe na Mzee Mitomingi. Miongoni mwa mliofanikiwa kupata nafasi ya kuhesabu watu,wapo mnaotumia pombe.wapo mtakaopelekwa katika vijiji vya mbali,huko ndio kwenye vishawishi zaidi. Pomnbe,Wasichana na mazingira kwa ujumla

Tunawatakia kilalakheri,tunaomba mtekeleze majukumu yenu vizuri kwa manufaa ya taifa letu.
Jiepusheni na vishawishi vinavyoweza kuharibu zoezi la sensa.lakini wakati tahadhari hii ikitolewa kwa maafisa,wazazi na walezi tunawaomba muwachunge watoto wenu hasa mabinti ambao wanaweza kuwa akina Binti Mazoea wasirubuniwe na vijana wa kiume watakaokuwa katika zoezi hili
Kwa bahati nzuri,wengi wao walioko mashuleni watakuwa katika mapumziko,mbali na kuwa kama akina Mazoea kuhatarisha Karatasi za Sensa,pia kuzuia Magonjwa ya zinaa na Mimba zisizotarajiwa

Tusikijukute taifa likipata watoto ambao hawakutarajiwa ambao majina yao yatashindikana kupatikana kwa haraka.Sijui wataitwa SENSA?
Vikao vya kamati za maandalizi ya Sensa bado vinaendelea.tafadhari Wenyeviti wa kamati hizo, Waratibu wa zoezi hilo sisitizeni umakini kwa maafisa wa Sensa. 
     nitumie maoni kupitia :juveilla@gmail.com

No comments:

Post a Comment