November 25, 2012

ngarakwetublogspot-Pius Ngeze Mfano wa Kuigwa Ngara




Ndugu zangu, 
Katika  pitapita zagu mitaa ya hapa Bukoba  nikalikuta Dukla la Vitabu. Hapo nikakikuta kitabu kiitwacho " Wanyonge Wasinyongwe". Mwandishi ni Bwana Pius Ngeze. Nilikisoma kwa siku moja tu. Na katika siku hiyo,jioni, nikakutana na mwandishi wa kitabu husika, Bw. Pius Ngeze.

Nilifahamu kuwa Pius Ngeze ni mwandishi wa vitabu na mara nyingine makala za magazetini. Lakini, kuongea na Pius Ngeze  ni sawa na kuingia darasani na kupata maarifa mapya yenye thamani kubwa. Huyu ni Mtanzania aliyeanza uongozi wa kisiasa akiwa kijana mdogo wa miaka 34.  Ni mwaka 1977 ndipo alipogombea na kushinda nafasi ya Uenyekiti wa Chama  ( CCM) mkoa wa Kagera.  Ngeze ni hazina kwa taifa kutokana na uzefu wake wa uongozi  kwa miaka mingi. Kwa sasa amestaafu uongozi wa kisiasa.

Baada ya kufahamu kuwa nimenunua na kusoma kitabu chake cha Wanyonge Wasinyonge, basi, Mzee Ngeze amenipa vitabu vyake vingine viwili; " Silaha 100 Za Kiongozi" na " Mwanzo Na Mwisho wa Uongozi Wa Kisiasa". Tumepanga tukutane tena ili tujadili yaliyomo kwenye vitabu hivyo na mengineyo. Inshalah.
Maggid Mjengwa,”

Ndugu mfuasi wa Blog hii. Hayo ni maneno ya Ndg Maggid Mjengwa aka Kiongozi napenda kumuita hivyo. Nakushawishi umfuatilie kupitia www.mjengwablog.com akizungumza kuhusu Mzee Pius Ngeze mzaliwa wa Ngara ambaye  Mdau JONAS KIZIMA aliyeko Chuo Kikuu cha SOKOINE  amenitumia taarifa kuwa katika mahafali ya 28 (yaliyofanyika 23 november 2012 morogoro campus ya mazimbu) ya chuo kikuu cha sokoine cha kilimo, kilimtunukia ndugu pius ngeze (mzaliwa wa wilaya ya ngara) nishani ya kutambua mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo kwa kufanikisha kuchapisha machapisho 57 yanaoelimisha katika sekta ya kilimo kwa lugha ya kiswahili na kingereza.

No comments:

Post a Comment