October 15, 2012

Matukio ya kujinyonga bado yapoNa Shaaban Ndyamukama Ngara
Mwanamke mwenye miaka 37 mkazi wa kijiji cha Buhororo wilayani Ngara mkoani Kagera amefariki dunia kwa kujinyonga akitumia kamba ya katani
Kaimu Mwenyekiti wa kijiji hicho Paulo Bwinyo alimtaja mwanamke  huyo kuwa ni Rejina Semitembe mkazi wa kitongoji cha Buhororo kati  ambaye alijinyonga jumatano majira ya saa tano mchana akiwa ndani ya nyumba.Bw Bwinyo alisema kuwa msichana huyo ambaye maishani mwake alikuwa bado kuolewa alipanda juu ya meza na kutundika kamba katika paa ya nyumba kisha kujitundika  baada ya kujifungia ndani ya  nyumba hiyo. Alisema wakati  wa uhai wake aliishi na mama yake mzazi mwenye zaidi ya miaka 70 na siku ya tukio mama yake alimuacha nyumbani na kuelekea shambani na aliporudi alikuta nyumba imefungwa  na alipowaita majirani walikuta mwanae huyo ameshafariki dunia
Naye shuhuda wa pili katika tukio hilo Bi Winifrida Thomas amesema mara baada ya mama wa marehemu kutoa taarifa kwa majirani kutaka msaada wa kufunguliwa nyumba yake walifika na kubomoa oukuta karibu na mlamgo wa nyumba na kumkuta msichana huyo akininginia sebuleni akiwa ameshafariki dunia
Bi winifrida amesema kuwa licha ya kuwa mzima siku za nyuma lakini tangu mwezi aprili mwaka huu alikuwa akidai kuwa na majini yanayomhubiri kutafuta kamba ili ajinyonge na alikuwa akiwaeleza watu kuwa iko siku atajinyonga bila kutoa sababu za kufanya hivyo
Mama yake mzazi na marehemu Bi Marcelina john alidai kuwa tangu aishi na mwanae alikuwa haoni tatizo lolote la kiafya au kuwa na msongo wa mawazo ispokuwa moyoni aliwaza kukosa mume kwani hakuna kijana wa kiume aliyewahi kumuona akiongea na binti yake katika masuala ya mapenzi
Jeshi la polisi wilayaniNgara limethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba linaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo.

1 comment:

  1. Duh! Inasikitisha sana. RIP, pole sana mama ulipotelewa na mwanao

    ReplyDelete