NA MWEMEZI MUHINGO KIBONDO
ZAIDI ya Abiria elfu mbili
waliokuwa wanasafiri kutoka mkoani Kigoma kuelekea mikoani wamekwama jana
kusafiri kwa saa tisa katika kijiji cha Kilemba wilayani kibondo baada ya mvua zinazoendelea
kuharibu Barabara
Sababu ya kukwama katika eneo hilo,
ni Gari kubwa lililokuwa limebeba mafuata kuingia kwenye tope na kushindwa
kupita kufunga njia na kuzuia magari mengine kupita.
Wakiongea kutoka katika eneo la
tukio baadhi ya abiria hao, walisema kuwa walikwama kuanzia saa mbili asubuhi
hadi kufika saa kumi walikuwa hawajui hatima ya safari yao itakuwaje
Aidha walisema kuwa maali walipo ni
porini hamna chakula wala maji ya kunywa na huku wana watoto wadogo wanapata
shida sana na uenda wakalala pale kama hautapatikana msaada wa haraka.
Juhudi za kulikwamua gari lililonasa
kwenye tope zilikuwa zinaendelea kwa msahada wa Vijana Jeshi la kujenga Taifa
Oparation miaka hamsini kikosi cha 824 KJ Kanembwa JKT japo hadi kufikia muda
wa saa kumi kulikuwa hakuna mafanikio yoyote.
Kaimu mkuu wa kikosi cha 824 kj
Kanembwa JKT, Captain, Thobias Ngailo alisema kuwa yeye baada ya kusikia kuwa
kuna magari yamekwama kwa
muda murefu na ni mengi aliamua
kupeleka kombania moja ya vijana kutoka kikosini hapo. na kuelekea katika eneo
hilo, kwakuwa moja ya kazi zao ni kusaidia jamii,ili kuhakikisha wanajaribu
kupunguza usumbufu wanao upata wasafiri na kuwashukuru, wananchi walioamua
kushirikiana na vijana wa jeshi hilo katika shughuli zote zilizokuwa zinaendelea
sehemu hiyo
Mmoja wa madereva wa mabasi yaendayo
mikoani, Salum Abdallah ambaye ni Dereva mabasi ya kampuni ya Adventure ya
mjini kigoma aliyekuwa anaelekea jijini mwanza, alipokuwa akiongea na Gazeti la
Mtanzania alisema kuwa Barabara inayokwenda kigoma kutoka nyakanazi imekuwa
mbovu siku nyingi na wao upata shida sana nyakati za masika.
Aidha alisema kuwa marakwa mara
wamekuwa wakilala njiani kwa sababu ya ubovu wa barabara na kuiomba serikali
kuutazama mkoa wa kigoma kwa kuwatengenezea barabara hiyo ili nawao wafanane na
mikoa mingine
Juhudi za kumtafuta meneja wa
Tanload Mkoa wa Kigoma Nalcis Choma ili azungumzie tatizo hilo,zilishindikana
baada ya simu yake ya mkononi kuwa haipatikani. Mwisho
Mwemezi Muhingo
P.O.BOX 160
KIBONDO
Mobile.0756906770
0789068612
Hii ndo kigoma yetu! full mitope na wahusika ni km hawaoni adha hii kwa wanancchi kwani kipande hicho cha kutoka nyakanazi hadi kigoma kimekuwa ni tataizo kwa muda mrefu bila ufumbuzi wa kiutendaji unaoonekana. Poleni sana ndugu zetu but "SERIKALI YETU NI SIKIVU HIVYO ITALIFANYIA KAZI SUALA HILO MAPEMA IWEZEKANAVYO"
ReplyDeletePoleni sana wana Kigoma
ReplyDelete