May 26, 2016

MFAHAMU AWILO LONGOMBA


Awilo Longomba alizaliwa huko Kinshasa, zamani ikifahamika kama Léopoldville. Baba yake alitokea katika mkoa wa Mongo-Ecuador, Mama yake pia ni mwenyeji wa huko katika Mkoa wa Ngombe ya Congo Brazzaville.

Awilo Longomba ni mwanamuziki wa Kongo ambaye alikuwa mpiga ngoma katika bendi za Viva la Musica, Stukas, Nouvelle Generation na Loketo.

Mwaka wa 1995, hatimaye aliacha kupiga ngoma na kuamua kuimba ambapo alitoa albamu yake ya kwanza, aliyoiita  Moto Pamba, baada ya kupata msaada kutoka kwa watu kama akina Shimita, Ballou Canta, Dindo Yogo, Dally Kimoko,Sam Mangwana, Syran Mbenza na Rigo Star.
Album yake ya pili, Coupe Bibamba aliitoa mwaka wa 1998ambayo  ilimfanya ajulikane kote barani Afrika, Ulaya na Amerika.

Hii ilifuatiwa na Kafou Kafou ya mwaka wa 2001 na albamu yake ya hivi karibuni, Mondongo  iliyotoka mwaka wa 2004, ambayo inawashirikisha akina  Japponais, Dally Kimoko, Caen Madoka, Djudjuchet, Josky na Simaro Lutumba.
 Pia alishirikishwa kama atalaku (mtu wa kutumbuiza) katika baadhi ya rekodi za soukous.
Awilo kwa sasa anaishi nchini Ufaransa .
AWlo amezaliwa katika Familia ya MUZIKI:-  Ikiwa ni  pamoja na baba yake Victor Longomba mwanachama mwanzilishi wa TP OK Jazz na vilevile Longombas ambalo ni kundi maarufu la afro-fusion lenye makao nchini Kenya.
Mnamo mwaka wa 2008 Awilo Longomba alitoa albamu mpya, ya SUPER-MAN, ambayo ilikuwa fanikio kubwa.
Awilo amefanikiwa kupata  umaarufu si Afrika tu, bali hata  Marekani / Kanada huku akiwa katika ziara pamoja na Nabtry International Cultural Dancers (kundi la kitamaduni la kimataifa la kusakata au kucheza ngoma) kundi la Kiafrika la kucheza ngoma lililoanzishwa mwaka wa 2007 na Grace Haukwa.

Awilo,kupitia Album yake ya Super Man amefanikiwa kupata  TUZO LA MTUMBUIZAJI BORA WA SOUKOUS WA MWAKA WA 2009.
 Penye nia,pana njia. Ni kwa jitihada kama alivyo fanya,amini inawezekana kufanikiwa.

No comments:

Post a Comment