October 15, 2012

Ntukamazina amwaga Msaada jimboni kwake



Na Shaaban Ndyamukama Ngara

Hospitali tatu na vituo vitatu vya Afya katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera zimepata msaada wa mshuka  380 kutoka Mfuko wa Bima ya Afya NHIF nchini kama moja ya hamasa kwa wagonjwa kuchangia mfuko huo na jamii kupata huduma za afya bila kutumia gharama kubwa za matibabu

Mbunge wa jimbo la ngara mkoani kagera Bw Deogratias Ntukamazina  alitoa mashuka hayo hivi karibuni wilayani Ngara  katika hospitali za Nyamiaga inayoendeshwa na serikali  kwa kuipatia mashuka 100 na mbili za binafsi za Murugwanza inayomilikiwa na kanisa Anglican  mashuka 100 pamoja na Hospitali ya Rulenge inayomilikiwa na kanisa katoliki jimboni humo nayo ilipata shuka 100

Bw Ntukamazina ambaye ni mwenyekiti wa bima ya afya Taifa alisema mashuka hayo  ni katika kuhamasisha jamii kuchangia na kutumia huduma ya bima ya afya kila kaya kwa kupunguza gharama za matibabu ambazo ni kubwa kuzimudu mtu mmoja kila kaya moja au kwa mtu binafsi kutokana na dawa kuwa pungufu katika Hospitali na zahanati

Aidha vituo vya Afya vya Bukiriro Mabawe na Murusagamba vilipata msaada wa mashuka 20 kila kimoja kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika vituo hivyo katika harakati za kupata matibabu na ambao wengi wao ni watoto chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito

Katika hatua nyingine mbunge huyo alitoa majaketi yanayoakisi mwanga nyakati za usiku kwa baadhi ya waendesha pikipiki katika wilaya ya ngara mkoani kagera ili kujikinga na ajali zisizo za lazima

Waendesha pikipiki walionufaika na msaada huo ni  kutoka vituo vya Rulenge Ngara mjini na Nyakisasa  ambapo mbunge alisema kuwa vijana wa maeneo hayo huzunguka maeneo mengi wilayani humo  na baadhi kupata ajali na kuhatarisha maisha yao

Alisema kuwa vijana hao wapatao 150 waliopata majaketi hayo kutoka NHIF  watakuwa kichocheo cha uhamasishaji wananchi kuchangia bima ya afya kwa kutoa shilingi 10000/= kila kaya kwa mfuko wa CHF na kutibiwa bure katika kadi ya watu watano.



No comments:

Post a Comment