June 3, 2013

Abiria elfu mbili wakwama kusafiri-Kibondo







NA MWEMEZI MUHINGO KIBONDO

ZAIDI ya Abiria elfu mbili waliokuwa wanasafiri kutoka mkoani Kigoma kuelekea mikoani wamekwama jana kusafiri kwa saa tisa katika kijiji cha Kilemba wilayani kibondo baada ya mvua zinazoendelea kuharibu Barabara

Sababu ya kukwama katika eneo hilo, ni Gari kubwa lililokuwa limebeba mafuata kuingia kwenye tope na kushindwa kupita kufunga njia na kuzuia magari mengine kupita.

Wakiongea kutoka katika eneo la tukio baadhi ya abiria hao, walisema kuwa walikwama kuanzia saa mbili asubuhi hadi kufika saa kumi walikuwa hawajui hatima ya safari yao itakuwaje

Aidha walisema kuwa maali walipo ni porini hamna chakula wala maji ya kunywa na huku wana watoto wadogo wanapata shida sana na uenda wakalala pale kama hautapatikana msaada wa haraka.

Juhudi za kulikwamua gari lililonasa kwenye tope zilikuwa zinaendelea kwa msahada wa Vijana Jeshi la kujenga Taifa Oparation miaka hamsini kikosi cha 824 KJ Kanembwa JKT japo hadi kufikia muda wa saa kumi kulikuwa hakuna mafanikio yoyote.

Kaimu mkuu wa kikosi cha 824 kj Kanembwa JKT, Captain, Thobias Ngailo alisema kuwa yeye baada ya kusikia kuwa kuna magari yamekwama kwa
muda murefu na ni mengi aliamua kupeleka kombania moja ya vijana kutoka kikosini hapo. na kuelekea katika eneo hilo, kwakuwa moja ya kazi zao ni kusaidia jamii,ili kuhakikisha wanajaribu kupunguza usumbufu wanao upata wasafiri na kuwashukuru, wananchi walioamua kushirikiana na vijana wa jeshi hilo katika shughuli zote zilizokuwa zinaendelea sehemu hiyo

Mmoja wa madereva wa mabasi yaendayo mikoani, Salum Abdallah ambaye ni Dereva mabasi ya kampuni ya Adventure ya mjini kigoma aliyekuwa anaelekea jijini mwanza, alipokuwa akiongea na Gazeti la Mtanzania alisema kuwa Barabara inayokwenda kigoma kutoka nyakanazi imekuwa mbovu siku nyingi na wao upata shida sana nyakati za masika.

Aidha alisema kuwa marakwa mara wamekuwa wakilala njiani kwa sababu ya ubovu wa barabara na kuiomba serikali kuutazama mkoa wa kigoma kwa kuwatengenezea barabara hiyo ili nawao wafanane na mikoa mingine

Juhudi za kumtafuta meneja wa Tanload Mkoa wa Kigoma Nalcis Choma ili azungumzie tatizo hilo,zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuwa haipatikani. Mwisho



Mwemezi Muhingo
P.O.BOX 160
KIBONDO
Mobile.0756906770
0789068612

2 comments:

  1. Hii ndo kigoma yetu! full mitope na wahusika ni km hawaoni adha hii kwa wanancchi kwani kipande hicho cha kutoka nyakanazi hadi kigoma kimekuwa ni tataizo kwa muda mrefu bila ufumbuzi wa kiutendaji unaoonekana. Poleni sana ndugu zetu but "SERIKALI YETU NI SIKIVU HIVYO ITALIFANYIA KAZI SUALA HILO MAPEMA IWEZEKANAVYO"

    ReplyDelete