July 23, 2012

CHADEMA TAWI LA NYAKIZIBA YAPATA OFISI


  Pichani hapo juu ni Katibu wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wilayani Ngara


Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Tawi la Nyakiziba wilayani Ngara kimepata ofisi yake baada ya kutokuwa na ofisi rasmi kwa miaka kadhaa tangu tawi hilo kuanzishwa

Ofisi hiyo imefunguliwa Rasmi Ijumaa iliyopita ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu wa CHADEMA wilayani Ngara mkoani Kagera Bw Cleophace Mudui huku umati mkubwa wa watu ukifurika 

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Ofisi hiyo, Katibu wa Chadema wilayani Ngara Bw Cleophace Mudui amewataka viongozi wa Chama hicho katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanawajibika ipasavyo katika kuwatumikia wanachama wao pamoja na wananchi kwa ujumla

Katika hatua nyingine Bw Mudui ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika nchini kuanzia tarehe 26 mwezi August

Amesema zoezi la sensa halibagui itikadi za kisiasa bali ni la watanzania wote na kwamba kila mmoja anapaswa kushiriki kikamilifu kwa maendeleo ya taifa zima

Ofisi iliyofunguliwa imegharimu kiasi cha shilingi laki 5 na elfu 70 katika ununuzi na ukarabati wake
Akisoma taarifa katika hafla ya ufunguzi wa ofisi hiyo, katibu wa Chadema tawi la Nyakiziba Bw John Kabiligi amesema kati ya fedha hizo shilingi laki mbili zimetumika kununua Ofisi hiyo wakati fedha za ukarabati ni shilingi laki tatu na elfu 70

Bw Kabiligi amesema kuwa kati ya fedha hizo shilingi laki nne zimetokana na michango ya wanachama na kwamba bado ukarabati haujakamilika

Wageni walioalikwa katika Hafla ya ufunguzi wa Ofisi hiyo walipata fursa ya kusaini Kitabu cha Wageni ndani ya ofisi ya chama hicho nami nilikuwa mmoja wao


Katika mkutano huo mmoja wa wanachama wanawake chama hicho mwanaharakati Bi Maryciana Zephania akawasisitiza wanawake kujitokeza kwa wingi kujiunga na chama hicho ambapo pia aliwataka wanawake wenye matatizo ya FISTULA kutojificha wala kufanya siri Uginjwa huo wanaodai kuwa wa Aibu kwa kuwa unatibiwa bure kwa sasa.

ngarakwetublogspot.com inamshukuru  Seif Omary Upupu wa sisipamojablogspot.com kufanikisha Habari hii
kwa habari/picha wasiliana nasi kupitia simu no.0713455929 au baruapepe juveilla@gmail.com


No comments:

Post a Comment