October 31, 2012

KAGERA YAZINDUA KAMPENI-OMAKA

Wauza mkaa Wilayani Biharamulo


BIHARAMULO

 Serikali mkoani Kagera inatarajia kufanya msako na kuwaondoa wavamizi wamisitu katika wilaya ya Biharamulo  kwa lengo la kuokoa mazingira katika operation maalumu ijulikanayo kama OMAKA

Zoezi hilo litakuwa chini ya uangalizi wa Mkuu wa Mkoa kanal mstaafu Fabian Massawe  kwakushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambo ni pamoja na jeshi lapolisi,magereza,TAKUKURU na Usalama wa taifa

Akitoa taarifa katika baraza la Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo,kwaniaba ya mkuu wa mkoa Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Lichard Mbeho amesema zoezi hilo litawahusisha watendaji wa serikali za Vijiji,wataalam wa Idara za ardhi,mifugo na Misitu

Amesema lengo kubwa ni kuhakikisha wavamizi wasio kuwa na Vibali wanakamatwa na kuondolewa katika maeneo hayo katika kata ambazo zina hifadhi ya misitu na wanyamapori

Bw. Mbeho ameyataja maeneo hayo kuwa ni Rusahunga,Nyakahura,Nyakanazi,Nemba, na kuhakikisha kuwa msako huo unafanyika kwa usalama bila uwangaji  damu

Aidha mkuu huyo wa wilaya ametoa rai kwa madiwani, na viongozi wengine ngazi za kata kutoa ushirikiano katika zoezi hilo ili kulinda na kuhifadhi mazingira

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Biharamulo Nassib Bakar Mbangga amesema uharibifu ni mkubwa unaotokana na wananchi kukosa uzalendo hasa ukataji wa miti na upasuaji wambao na ujangiri katika pori la Burigi

Imeelezwa kwamba katika mji wa Biharamulo na maeneo jirani magunia zaidi ya 600 yanauzwa kila siku kwa kutembezwa na wapanda Baiskeli na Tani mia sita kwa mwezi za mkaa na Mbao huuzwa wilayani humo na hata nje ya mkoa na wakati mwingine nje ya Nchi hasa Rwanda na Burundi

Amesema watendaji wake wanafanya kazi bila uadirifu wakitumia mianya ya rushwa kwa vyeo vyao kuwagawia maeneo wafugaji kutoka nje ya wilaya hiyo pamoja na wale watokao nje ya Nchi

Aidha Mkurugenzi huyo amesema hatamuonea aibu mtumishi yeyote wa umaa atakayekiuka taratibu, kwakumchukulia hatua mbali mbali za kisheria na kwamba watum,ishi hao watoe huduma kwa jamii kulingana na taaluma zao kwa kutembelea wanachi vijijini na kuepuka kuwa vyanzo vya majungu

No comments:

Post a Comment