October 23, 2013

CHADEMA NGARA WAMCHAGUA ALIYEKUWA MWENYEKITI NCCR MAGEUZI





-MWENYEKITI CHADEMA KAGERA:-HAKUNA KIZUIZI KWA CHADEMA KUINGIA IKULU
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilayani Ngara kimemchagua aliyekuwa mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Bw.Kennedy  Stanford kuwa mwenyekiti wa chama hicho
Bw.Stanford ameukwaa uenyekiti huo,kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wilaya ya Ngara Mkoani Kagera kufanya uchaguzi na kupata viongozi wa kikatiba watakaokiongoza chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani

Katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 19,2013 katika ukumbi wa Paradise mjini Ngara na kusimamiwa na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kagera Bw. Wilfred Lwakatare, mwanachama mpya wa chadema Bw Kenedy Stanford ambaye alihamia rasmi CHADEMA mwezi  August mwaka huu na kukabidiwa kadi ya uanachana na mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh. Freeman Mbowe  amechaguliwa kuwa mwenyekiti baada ya kujiuzulu kwa Bw Essau Hosea Chiza

Nafasi ya Katibu imechukuliwa na Bw Filmon Charles huku Bw Nestory Mashishanga akibaki katika nasafi yake ya mwenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho na Katibu mwenezi akibaki Bw Wilson Kakoko

Aidha uchaguzi huo umehudhuriwa na wajumbe 103 kutoka kata 17 kati ya 20 za wilaya ya Ngara ambao wameshiriki kupiga kura kwa viongozi hao
Akizungumza baada ya Uchaguzi huo,mwenyekiti wa Chadema Mkoani Kagera Bw. Wilfred Mugisha Lwakatare amesema kupatikana kwa viongozi waliochaguliwa kutaimarisha nguvu ya chama hicho na kuhakikisha ushindi katika uchaguzi mkuu ujaop kuanzia ngazi za vijiji ,kata,jimbo na uraisi

“Hakuna kizuizi tena kwa CHADEMA kwenda Ikulu,miongoni mwa maeneo ambayo CHADEMA Haikuwa na nguvu sana ni Ngara. Ila kwasasa Chama hiki kimeshika kasi,na kufikia uchaguzi mkuu tutakuwa na nguvu zaidi,kwahiyo ushindi ni wa CHadema kwa ngazi zote” alisema

Aidha,Bw. Lwakatare amewapongeza wanachama wa chama hicho kwa namna wanavyojitoa kuimarisha chama chao,akiongeza kuwa hata katika uchaguzi huo wajumbe wamejisafirisha kwenda na kurudi,bila kudai posho

No comments:

Post a Comment