December 16, 2017

UCHAGUZI WA ANC,AFRIKA YA KUSINI

Ramaphosa, Dlamini-Zuma kuwania uongozi wa ANC

SOURCE:DW
Chama tawala nchini Afrika kusini,  ANC kinafanya uchaguzi mwishoni mwa juma, unaoonekana kuwa mgumu, kumchagua mrithi wa kiongozi wake Jacob Zuma, ambapo mshindi  pia atakuwa na nafasi ya kuwa  rais mpya wa nchi hiyo.
Bildkombo Nkosazana Dlamini-Zuma und Cyril Ramaphosa (Getty Images/AFP/R. Jantilal/G. Kirk)
Chama  cha  ANC  kitamtangaza  mrithi  wa  rais  wa  sasa  Zuma kuwa  kiongozi  wa  chama  Jumapili (17.12.2017), kikikamilisha mpambano  mkali  wa  kuwania  uongozi  ambao unatishia  kukigawa chama  hicho  ambacho  kilianza  kama  vuguvugu  la  ukombozi miaka  105  iliyopita, ambacho  kimekuwa  madarakani  tangu mwaka  1994.
Makamu  wa  rais Cyril Ramaphosa , mwenye  umri  wa  miaka 65, ambaye  kwa  kiasi kikubwa  anapendelewa  na  masoko  ya  fedha, na  Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenye  umri  wa  miaka  68, waziri  wa  zamani  na mwenyekiti  wa  halmashauri  ya  Umoja  wa  Afrika  wametamalaki katika  mpambano  huo.
Cyril Ramaphosa Südafrika Wahlen (DW/A. Lattus)
Makamu wa rais Cyril Ramaphosa
Sarafu  ya  Afrika  kusini  ya  rand imekuwa  imara  kwa  asilimia mbili  baada  ya  mahakama  kutoa  hukumu  kwamba maafisa waandamizi  katika  majimbo  mawili walioonekana  kumuunga mkono  Dlamini-Zuma walichaguliwa  kinyume  na  sheria  na hawataruhusiwa  kuhudhuria  mkutano  huo.
"Ishara  za  mapema za ushindi  kwa  Cyril Ramaphosa, ambaye anapendelewa  na  wawekezaji  zaidi, ametoa  usaidizi kwa  sarafu ya  rand," John Ashbourne , mtaalamu  wa  uchumi  wa  Afrika  katika taasisi  ya  Capital Economics  amesema.
"Lakini  wakati Ramaphosa anaungwa mkono  kwa  kiasi  kikubwa miongoni  mwa  wanachama  wa  chama  hicho, matokeo yataamuliwa  na  watu  wa  ndani kisiasa, ambao  huenda wakaamua  kumuunga mkono  mpinzani  wake mfuasi  wa  siasa  wa mrengo  wa  kushoto, Nkosazana Dlamini-Zuma.
Dlamini-Zuma (Getty Images/AFP/F. Monteforte)
Nkosazana Dlamini-Zuma
Ramaphosa  alishinda  kwa  wingi  wa  kura  za  kuteuliwa  kuwa kiongozi  wa  chama, lakini  wajumbe  katika  mkutano  huo ulioanza JumamosiDisemba  (16-12  hadi 20.12.2017) mjini  Johannesburg hawafungwi na kura alizopigiwa  na  tawi la  chama  cha  ANC lililomteua  kuwa  mgombea  wao, ikiwa  na  maana  kwamba  bado haiko  wazi  iwapo  anaweza  kushinda  nafasi  hiyo.
Ramaphosa  ameongeza  hivi  karibuni  ukosoaji  wa  serikali  ya Zuma  iliyogubikwa  na  kashfa, wakati Dlamini-Zuma  amesema umuhimu   wake  anauweka  katika  kuboresha  uwezo  wa  Waafrika waliowengi.
Waungaji mkono Ramaphosa
Kwa  waungaji  wake  mkono, mafanikio  ya  Ramaphosa  kibiashara yanamfanya  kuwa  katika  nafasi  nzuri  ya  jukumu  la  kubadilisha hali  ya  uchumi  wa  nchi  hiyo  inayokabiliwa  na  ukosefu  wa nafasi  za  ajira  kwa  asilimia  28  ya  watu pamoja  na kupunguziwa viwango  vya  uwezo  wa  kukopa.
Südafrika Zuma hält Rede im Orlando Stadion in Soweto (Getty Images/AFP/M. Safodien)
Mkutano wa ANC akihutubia mwenyekiti Jacob Zuma
Kwa upande  mwingine, Dlamini-Zuma anaonekana  kuwa  mpiganaji imara  dhidi  ya  kutokuwa  na  uwiano  wa  Waafrika  na  wazungu hali  ambayo  uhasama  wake  unaoelekezwa  katika  makampuni makubwa  umewatisha  wawekezaji   nchini  Afrika  kusini.
"Matokeo  ni  vigumu  kutabiri. Hii  inaleta  hali  mbaya  ya sintofahamu  ambayo  inaakisi  kwa  kiwango  kikubwa  hali  mbaya ya  sarafu  ya  rand, " Elizabeth Andreae, mchambuzi  katika  benki ya  Commerzbank  amesema  katika  taarifa.
Ukuaji  wa  uchumi  katika  taifa  hilo  lenye  uchumi  mkubwa  wa viwanda  barani Afrika umekuwa  wa  kusua sua  kwa  miaka  sita iliyopita, na  kiwango  cha  watu  wasio  na  kazi  inakaribia  viwango vya  juu  kabisa.
Wachambuzi  wanasema  kinyang'anyiro  cha  kuwania  uongozi  wa ANC  umefanya  hali  kuwa  ngumu  kuweza  kufanya  mabadiliko  ya kiuchumi  na  kuboresha  huduma  za  jamii.
Ruanda Rede Nkosazana Dlamini-Zuma Sitzung AU Gipfel (picture-alliance/Photoshot/P. Siwei)
Rais wa zamani wa halmashauri ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma
Zuma alitoa utani  katika  chakula  cha  usiku  kwa  wajumbe  wa ANC katika  mkesha  wa  mkutano  huo  mkuu  na  kusema  kwamba "imekuwa uzoefu unaostahili" na  kwamba  anasubiri  kwa  hamu kuondoka  madarakani  kama  kiongozi. Anatarajiwa  kutoa  hotuba yake  ambayo  si  rasmi  sana  mwanzoni mwa  mkutano  huo  mkuu wa  chama. Anabakia  kuwa  kiongozi  wa  taifa  hadi  2019.
Rais  huyo  mwenye  umri  wa  miaka  75 amekana  madai  kadhaa ya  rushwa  tangu  alipoingia  madarakani  mwaka  2009  na amenusurika  mara  kadhaa  katika  kura  za  kutokuwa  na  imani nae  bungeni.
"Watu wanasubiri  kwa  hamu  kuondoka  kwake," mchambuzi  wa masuala  ya  kisiasa  Prince Mashele  amesema  katika  taarifa yake  aliyoiandika  katika  gazeti  moja.
Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre
Mhariri: Isaac Gamba
www.ngarakwetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment