August 16, 2012

Koffi Olomide apiga

Mwanamuziki mkongwe wa Lingala nchini DRC Koffi Olomide anashitakiwa kwa kumpiga Mtayarishaji wake wa muziki.

Koffi alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani  jana baada ya kuzuka vurugu katika hoteli moja mjini Kinshasa.

Inadaiwa kuwa kesi hiyo imevutia umati mkubwa wa watu mjini Kinshasa uliofurika mahakamani hapo kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.

Kesi hiyo iliharishwa hadi leo asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.

Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide aliwakilishwa na mawakili 10.

Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishaji wake Diego Lubaki, umetokana na kudaiana dola $3,680.

No comments:

Post a Comment