July 13, 2014

LIONEL MESSI APEWA TUZO YA MCHEZAJI BORA KOMBE LA DUNIA 2014

Lionel Messi kulia,amepewa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano .
LICHA ya kupoteza mechi ya fainali na kukosa kombe la dunia mwaka 2014, mshambuliaji wa Argentina na Barcelona, Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya kombe la dunia mwaka huu 2014nchini Brazil.
wachambuzi wa masuala ya Soka wanasema  Messi alionesha kiwango kikubwa katika hatua ya makundi akifunga mabao 4 katika michezo mitatu dhidi ya Bosnia, Iran na Nigeria, lakini nyota yake ilififia baada ya kushindwa kufunga katika mechi za mtoano dhidi ya Switzerland, Ubelgiji, Uholanzi na Ujerumani.
Katika mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumani, Messi alipoteza nafasi moja muhimu, lakini muda mwingi alifanya jitihada za kutafuta upenyo bila mafanikio. 

No comments:

Post a Comment