October 15, 2012

TAARIFA KWA UMMA

                                               TAARIFA KWA UMMA
Kwa niaba ya chama cha mpira wa miguu wilaya ya Ngara, napenda kutoa pole kwa uongozi wa Klabu ya soka ya Rusumo Fc, wachezaji, wapenzi na mashabiki wa soka wilaya ya Ngara, ndugu pamoja na jamaa wote kufuatia ajali ya gari lililokuwa limewabeba mashabiki wa timu hiyo waliokuwa wakitoka kwenye mechi ya kusaka timu ya kuingia hatua ya robo fainali ya michuano ya polisi Jamii wilayani Ngara.

Ajali hiyo imetokea jana majira ya kati ya saa 1:30 hadi saa 2 usiku katika eneo Zerozero ambapo waliofariki hadi sasa ni watano huku wengine 22 wakijeruhiwa na kulazwa kwenye Hospitali Teule ya Murgwanza

Chanzo cha ajali hiyo iliyolihusisha gari la polisi lililokuwa limewabeba mashabiki hao ni kumulikwa na mwanga mkali wa taa za Lori la Mizigo walilokuwa wakipishana nalo hali iliyosababisha gari hilo kuligonga jiwe lililokuwa pembezoni mwa barabara na kupasuka Gurudumu na kisha kupinduka
Chama cha Mpira wa miguu wilaya ya Ngara kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali na vifo vya mashabiki hao na tunatoa pole kwa wafiwa, hasa klabu ya Rusumo fc, Ndugu wa marehemu na wapenzi wa soka wilayani Ngara kwa ujumla pamoja na Jeshi la Polisi ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo, pia tunawaombea heri Majeruhi waweze kupona haraka na kurejea katika shughuli zao za ujenzi wa Taifa

Mungu ibariki Rusumo Fc, Mungu Ibariki Ngara, Mungu Ibariki Tanzania

SEIF OMARY "UPUPU"
MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA WILAYA NGARA

No comments:

Post a Comment