October 28, 2012

Vijana tafuteni elimu kwa kutanguliza dira katika maisha

Askofu wa Jimbo Katoliki Rulenge-Ngara Severin Niwemugizi,akiwa na Dr peter Bujari Mkurugenzi wa HDT katika mahafali ya 30 kidato cha nne katika shule ya sekondari Mt. Alfred Rulenge


Vijana tafuteni elimu kwa kutanguliza dira katika maisha
Na, Shaaban Ndyamukama –www.ngarakwetublogspot.com
Vijana wametakiwa kujiwekea dira ya maisha katika kutafuta elimu ili kukabiliana na ushindani wa kupata ajira duniani na kupambana na utandawazi kwa lengo la kudumisha maadili ya kwenye jamii zao.
Mkurugenzi wa HDT mkoani Kagera Dr peter Bujali ametoa kauli hiyo  katika  mahafali ya 30 ya kidato cha nne kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mt Alfred Rulenge(RAMA) iliyoko wilayani Ngara. Dr Bujari amesema kuwa  vijana wengi wanashindwa kutimiza  ndoto za maisha  kwa kuwa hawana malengo  wakati wakitafuta elimu na hatimaye kukosa mwelekeo wa maisha yao na kuendelea kuwa maskini
Amesema kuwa dira hizo ziambatane na kuwajibika ipasavyo katika kutafuta taaluma kujenga uaminifu katika utumishi nakukuza uchumi pamoja na kudai haki bila kuhatarisha amani. Aidha Dr Bujali amesema mafanikio ya vijana yatapatikana endapo  watafuata miiko na kulinda maadili ya jamii kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na mamlaka iliyo juu yao
Alisema mataifa mengi yamekumbwa na vurugu za kuvunjika kwa amani baada ya kukiuka taratibu na maadili pale wanapopatikana watu wasiostahili nafasi zao kwa kutumia udini ukabila na udugu unaopelekea  kukiuka haki wajibu na sheria
Alisisitiza vijana kuwa wanao wajibu wa kutafuta taaluma kwa juhudi na maarifa ili kujikomboa na umaskini kwa kushirikiana na wazazi au walezi wao wakiwemo walimu ili kuhakikisha wanafaulu maisha wakiepuka tamaaza mahitaji wasiyo na uwezo nayo

No comments:

Post a Comment