October 28, 2012

DC Ngara atoa agizo kwa wazazi kuhusu Elimu

Mkuu wa wilaya ya Ngara Constantine Kanyasu


    DC Ngara atoa agizo kwa wazazi kuhusu Elimu
Na: Shaaban Ndyamukama –ngarakwetublogspot.com
Mkuu wa wilaya ya ngara mkoani Kagera Bw Costantine Kanyasu amewataka wazazi kufanya maadalizi ya kuwaendeleza watoto wao kielimu mara watakapochaguliwa baada ya kufaulu mitihani yao 
Bw Kanyasu ametoa kauli hiyo alhamisi wiki hii katika mkutano wake na wakazi wa kata ya Nyamiaga wilayani Ngara wakati wa mahafali ya 27 ya darasa la saba katika shule ya msingi Kumuyange
Amesema wazazi wanalo jukumu la kuwalea watoto wao na kuwaendeleza kielimu ili kukabiliana na ushindani wa ajira katika shirikisho la afrika ya Mashariki kuliko kukaa nyumbani na kushindwa kazi za vibarua katika shirikisho hilo
Amesema ni jambo la aibu kwa serikali ya Tanzania kuwa vijana wasiojitambua kielimu na kuendelea kuwa maskini wakati nchi hii imejaa rasilimali nyingi za kuweza kielimu  kutumika katika kuwekeza kwa kuwapeleka vijana kwenye shule mbalimbali na kujifunza fani za kuwasaidia kimaisha
Amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha wanafunzi wanaochaguliwa kuingia sekondari au elimu ya juu wanakwenda  na wazazi watakao kwamisha juhudi hizo vyombo vya dola vitamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafungulia mashtaka mahakamani
Picha ya dc
Katika hatua nyingine baadhi ya wadau  wa elimu  katika wilaya ya Ngara mkoani  wamependekeza serikali kubadili utaratibu wa kutoa mitihani ya kuhitimu elimu yamsingi  kwa mfumo wa kuchagua majibu yenye herufi sahihi  kwa kuwa mfumo huo  unapoteza vipaji vya wanafunzi kujieleza kwa kuandika .Meneja wa shule ya msigi na sekondari  ya  RHEC  wilaya ya Ngara ambaye alikuwa  ni mwenyekiti wa CCM wilayani humo  Bi Helena Adrian alisema mabadiliko ya mara kwa mara katika mitaala ya elimu  nchini ni moja ya changamoto inayoikabili sekta ya elimu ambapo walimu na wanafunzi wa shule za sekondari za serikali na watu binafsi kushindwa kutoa taaluma inayokubalika na kuwa katika ushindani ndani ya afrika mashariki. Alisema kuwa mitihani ya kuchagua imebainika kuwa na dosari kwa baadhi ya wanafunzi kufaulu masomo kwenda ngazi nyingine  ya elimu wakiwa hawana taaluma inayokubalika na kuwapa wakati mugumu walimu kufundisha mada ambazo hutumia muda mwingi kuzifanyia marudio katika kufundisha wanafunzi wasiojua kusoma wala akuandika.
Naye Katibu wa  mbunge wa jimbo la Ngara mkoani Kagera kupitia CCM Bw Ruguge Nzutu Ruguge alisema   kuwa kubadilika kwa mitaala kunawafanya wanafunzi wa ngazi za elimu kutofautiana katika kufanya mitihani ikiwa ni pamoja na lugha za kufanya mitihani hiyo kuhitilafina. Ruguge alisema kuwa wapo wanafunzi wa shule binafsi kama Englis Medium kufanya masomo yao kwa lugha ya kiingereza na wengine wa shule za msingi kutumia kiswahili katika kujifunza na kusababisha matabaka katika utoaji wa elimu ndani ya kaya au katika jamii moja
Alisema kuna haja ya watunga sera za maendeleo ya taaluma kubadili mfumo wa elimu ili kila mmoja apate elimu kwa kiwango kinachorandana na mazingira yake kuliko kuiga sera za wageni na kuwa tegemezi katika taifa hatimaye kuwa na wataalamu wasiojiweza kutafsri sheria na mikataba
Alidai serikali itoe tamkoa la lazima la kuwanusuru  watoto wengine ambao hushindwa kupata elimu  na kubaki mitaani wakiwa ombaomba na kukiuka kauli mbiu ya mwalimu Nyerere ya kupata elimu kwa wote
Hawa ni watoto  wa mukibungere kata ya mabawe wilayani Ngara ambao  wamekosa haki yao ya kupata elimu
Katika tathmini ya elimu nchini kwa wadau hao  mkuu wa wilaya ya Ngara  Costantini Kanyasu aliwahimiza wahitimu wa  ngazi za elimu wilayani humo kuwa waadilifu katika jamii kwa kutumia elimu yao kufanya matendo yanayokubalika kisheria na kuwa mfano bora kwa wale waliokwepa kwenda shule
Kanyasu alisema wazazi wanao wajibu mkubwa wa kutoa elimu kwa watoto wao kwapatia elimu kwa kukwepa kulipia gharama za mafunzo kwa kuwa elimu ni kuwekeza na ni mtaji wa familia endapo watakuwa karibu kufuatilia kile mwanafunzi anachopata shuleni
‘’Kamawazazi mtawajibika na kulipa karo kwa wakati kisha mkawa ni wafuatiliaji wazuri wa watoto wenu katika taaluma na wanafunzi kwa namna yoyote  wataweka bidii ya kujifunza hatimaye kufanikiwa malengo yao na kuongeza uadilifu kwa matendo yenye nidhamu.” Alisema Kanyasu
 Alidai kuwa serikali haina nafasi za ajira za kutosheleza maelfu ya wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kilichopo ni kujifunza fani zitakazowasaidia kujiajiri ili kujikwamua kimaisha kwa kuanzisha ujasiliamali ulio na taaluma ndani yake kupambana na umaskini katika familia na jamii kwa ujumla.
Aidha aliwataka wahitimu wa kidato cha nne  kutumia elimu na maadili waliyopewa na walimu wao kuandaa mazingira ya kuwa viongozi bora na watangulize uwajibikaji kwa watakao pata ajira katika taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi.
No comments:

Post a Comment