October 28, 2012

Wananchi waomba kuboreshewa Gulio wilayani Ngara

Baadhi ya wakazi wa mji wa kabanga-Ngara wakiwa gulioni


Na: Shaaban Ndyamukama Ngara
Wakazi wa mji wa kata  Kabanga wilaya ya Ngara mkoani Kagera wameiomba halmashauri ya wilaya hiyo kuwapatia uwanja maaluma kwa ajili ya soko  na kujenga chanja za kuuzia mazao yao  badala ya kuyauzia chini ya udongo
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi katika  mji huo  jana wananchi hao walisema kuwa wanafanya biashara ya kuuza matunda na vyakula vibichi katika soko dogo karibu na  mashamba ya watu  na kushindwa  kuboresha biashara kwa wateja katika kuinua kipato
Mmoja wa wakazi wa mji huo  Sarafina Maulidi alisema kuwa serikali haina budi kuandaa uwanja wa soko na wafanyabiashara kujenga vibanda  na chanja za kuwekea bidhaa zao ikiwa ni pamoja na kujikinga na maradhi ya kipindupindu hasa wakati wa mvua kali
Sarafina alisema katika kupanga gulioni lisilotosheleza wakazi wa mji huo hulazimika kulipa shilingi  100 kwa ajili ya kumlipa mtu anayefanya usafi lakini fedha hizo ni nyingi kwa kila mwenye bidhaa na vinywaji vya asili  na zinapaswa kutumika kwa ajili ya kuchimbia mashimo ya takataka pamoja na choo cha soko
 Kwa upande wake Saidi Manywele alisema wananchi wanapata shida  kwa kuwakiwa na jua kali ama kunyeshewa na mvua hivyo panahitaji uboreshaji wa masoko wilayani Ngara

Alisema pia licha ya serikali kupiga marufuku wakulima kuwatoza ushuru  wa mazao  yapelekwayo gulioni kama viazi  ndizi na mboga mboga bado watendaji wa halmashauri ngazi ya kata wanaendelea kuwasumbua watu hao na kuwa kero ndani ya jamii 
Naye Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ngara  Simon Mumbee alisema kwamba vipaumbele vya wananchi hupangwa na kamati ya maendeleo ya kata WDC na kama watahamasishwa kupata soko la kisasa halmashauri iko tayari kutekeleza matakwa yao

No comments:

Post a Comment