November 22, 2012

LIPUMBA-CCM IMESHINDWA KUWATETEA WANANCHI

Mwenyekiti wa CUF taifa- Prof. Ibrahim Haruna Lipumba


Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Taifa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amekitabilia vibaya ma Chama cha Mapinduzi CCM kilichoko madarakani hivi sasa kuwa kitaanguka katika uchaguzi mkuu wa 2015 kwa madai kuwa kimeshindwa kuwaletea maendeleo Wananchi

Prof. Lipumba amesema hayo jana wakati akizungumza na Waandishi wa habari wilayani Kibondo Mkoani Kigoma baada ya kuwaslili wilayani humo akitokea Mjini kigoma akihitimisha ziara yake Mkoa ya Kigoma

Amesema CCM kwa sasa kina baadhhi ya Viongozi ambao si waadilifu,wala rushwa na waliopo madarakani kwa maslahi yao bnafsi hivyo wanakichafua chama hicho hali inayopelekea wananchi kukosa imani

Ametolea mfano Vitendo vya Rushwa ambavyo vimekuwa vikiripotiwa kwa nyaakati tofauti hasa katika chaguzi mbali mbali ikiwa ni pamoja na Uchaguzi ndani ya Chma hicho uliomalizika hivi Karibuni

Kutokana na hayo, Prof Lipumba Amesema Vyama vya Upinzani Nchini havina budi kuunganisha Nguvu kujenga Umoja wa kitaifa, na kujipanga sawasawa ili kuhakikisha wanakidondosha Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi uja akidai kuwa  kimeshindwa kutetea maslahi ya wananchi

Aidha, Prof Lipumba amesema kuwa CCM kimeshindwa kutimiza ahadi zake kwa wananchi hali ambayo imepelekea mgawanyiko kati ya wenye mali na Masikini kwa maana ya kuwepo daraja la wenye nacho na wasiokuwa nacho

Ameongeza kuwa dawa pekee ya kusuluhisha changamoto zinazowakabili Watanzania ni kuhakikisha Chama pinzani kinaingia madarakani.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa Chama cha wananchi CUF Taifa akisema kuwa anaongozwa na falsafa ya chama chake Vision 4 Change au Ndoto ya mafanikio amesema Taifa la Tanzania lina rasilimali nyingi ingawa watanzania walio wengi wanaishi katika maisha ya Kimasikini

Prof. Lipunmba amesema njia ya kuwakomboa watanzania wengi ni kupitia Sekta ya kilimo kwa kuboresha mfumo uliopo hivi sasa

Amesema Serikali imejaribu kubuni njia za kuboresha kilimo  kwa kutamburisha matumizi ya matrekta madogo maarufu kama power tillers, Pembejeo  na Mbolea ya Ruzuku lkn bado kuna changamoto nyingi kwa kuwa matrekta hayo sehemu kubwa hayafai kutokana na arhi ya sehemu husika, na Mbolea kuto wafikia walengwa ipasavyo
Kutokana na maelezo ya Prof lipumba, ili serikali itemize falsafa ya Kilimo Kwanza haina budi kutumia asilimia 10 ya bnajeti yake ya matumizi yake

Amesema kwa mujibu wa makubaliano ya Nchi za SADC zilikubaliana kuwa serikali za Nchi wanachama zinatakiwa kutenga asilimia 10 ya matumizi yote ya serikali katika sekta ya Kilimo lakini Tanzania bado haijafanya hivyo

Aidha,mwenyekiti huyo amesema ili kubooresha sekta ya kilimo Serikali pia haina budi kuweka vituo vya utafiti wa Kilimo vijijini ili kuwafikia wakulima na kulaani vikali matumizi mabaya ya fedha zinazotengwa kwaajili ya pembejeo za Kilimo kwani hazitumiki ipasavyo na badala yake wapo Viongozi wa Serikali wanaotumia fursa hizo kujinufaisha binafsi.    Kwa maslahi yao binafsi. Mwisho

No comments:

Post a Comment