November 26, 2012

MSANII SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA




Sharlo Millionaire enzi za uhai wake



Habari zinaeleza kuwa kifo chake kimetokea Novemba 26(Jana) majira ya saa mbili usiku, ambapo msanii huyo wa Muziki wa Kizazi kipya maarufu kama Bongo flavour  na mchekeshaji maarufu nchini Sharo Milionea amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari wakati akitoa Dar es Salaam kueleka wilayani Muheza, Tanga.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe Hussein Ramadhani au Sharo Milionea alikuwa akiendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier. Alipofika maeneo ya Segera gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa, likagonga mti na kusababisha kifo chake na yeye kutokea mbele ya kioo cha gari na kutupwa mbali.
Alisema Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza. Aliongeza kuwa hakuna kona kali wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali. Gari lake imehifadhiwa mahali salama kwakuwa limeharibika vibaya na kwamba kwenye gari alikuwa mwenyewe.


Mwili wa marehemu baada ya ajali




Habari kuhusu kifo chake zilianza kuenea jana usiku ambapo kwa upande wa rafiki yake wa karibu Kitale amesema alikuwa akiipiga simu ya Sharo Milionea iliyokuwa ikiita kwa muda mrefu bila kupokelewa na kisha kupigiwa simu na Tundaman, Mzee Majuto na Mjomba wake Sharo kumtaarifu juu ya kifo hicho.

“Sisi binadamu tunaweza kuwaza hivi na Mungu naye akawaza lake kwahiyo sisi tunaziombea familia hizi Mungu azipe faraja ya kweli na faraja ya kweli nadhani inatoka kwa Mungu,” ni kauli ya rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania , TAFF Simoni Mwakifwamba wakati akizungumza na Shirika la Utangazaji hapa Nchini TBC.

Umoja wasanii wa filamu nchini umesema umepata pigo kubwa hasa kwakuwa bado wana msiba wa msanii mwingine wa filamu, John Stephano ambaye anatarajia kuzikwa leo. Umesema baada ya mazishi hayo kesho watasafiri kwa mabasi mawili kuelekea wilayani Muheza kwaajili ya mazishi.

   Mungu ailaze mahali pema pepon roho ya Marehemu-Amen
 Tunaomba radhi,picha zinatisha hazistahili kuwekwa wazi


No comments:

Post a Comment