November 2, 2012

RUSUMO-Maporomoko yatakayozalisha Umeme

Maporomoko ya Maji-Rusumo-Ngara


Na:- Juventus Juvenary-Ngara

Pichani hapo juuni  Maporomoko ya maji, yaliyopelekea SERIKALI ya Tanzania, Burundi na Rwanda kutiliana saini mkataba wa maridhiano ya pamoja katika kusimamia mradi mpya na mkubwa wa kuzalisha umeme, kwenye maporomoko ya maji katika Mto Ruvbu uliopo Mkoa wa Kagera hapa nchini.
Mradi huo uliopo chini ya Uratibu wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki (EAC), umefadhiliwa na Benki ya Dunia (WB), na unatarajia kuzalisha megawati 90 za nishati ya umeme, na kwamba kila nchi itapata megawati 30 katika mradi huo mkubwa.

Mkataba huo wa pamoja ambao umetiliwa saini jijini Mwanza, umelenga kuchochea zaidi ukuaji wa maendeleo na kupunguza tatizo la upatikanaji wa nishati hiyo, hivyo wanannchi wan chi husika watanufaika na umeme huo
Mkataba huo wa pamoja, umesainiwa na Mawaziri wa nchi hizo wanaoshughulikia masuala ya Nishati ambao ni Waziri Ngeleja wa Tanzania, Waziri wa Nchi, Maji na Nishati wa Rwanda, Emmanuel Isumbingabu pamoja na Waziri wa Burundi anayeshughulikia masuala ya Nishati, Maji na Madini, Manirakiza Come.
Waziri Ngeleja aliyataja maeneo hapa nchini yatakayonufaika na mradi huo wa umeme utokanao na maporomoko ya Mto Rusumo, kuwa ni pamoja na wilaya ya Sengerema na Geita (Mwanza), Kibondo na Kasulu (Kigoma), pamoja na maeneo ya Mkoa wa Kagera.

No comments:

Post a Comment